Kipigo cha mabao 2-1 ilichokipata Liverpool juzi kutoka kwa Paris St-Germain, kimeiweka katika nafasi finyu ya kufuzu hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Hii ni mara ya kwanza kwa Liverpool kupoteza mechi nne mfululizo za ugenini katika michuano ya Ulaya, lakini kocha Jurgen Klopp, anajipa matumaini kuwa wanayo nafasi ya kufuzu.
Kocha huyo raia wa Ujerumani, alisema watahakikisha wanaishinda Napoli kuanzia mabao 2-0 watakapoialika katika mchezo wa mwisho wa makundi utakaofanyika mwezi ujao kwenye Uwanja wa Anfield.
Ni matokeo mabaya tuliyoyapa leo ‘juzi’ lakini siamini kama yamemaliza ndoto zetu za kuingia hatua ya mtoano, tunaweza kushinda mabao 2-0 Anfield, tunacho kikosi imara acha tusubiri kuona,” alisema.
Upande wa pili ushindi umeifanya PSG kuboresha rekodi ikishinda mchezo wa 21 nyumbani katika hatua ya makundi bila kupoteza mara ya mwisho kupoteza nyumbani ni Desemba 2004walipofungwa 3-1 na CSKA Moscow.
PSG imekuwa timu ya tatu kushinda mechi nyingi za nyumbani katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, imeshinda 50 kati ya 95 ilizocheza, timu zilizoshinda mechi nyingi zaidi ni Real Madrid 88 na Barcelona 93.
Tangu msimu wa mwaka 2016-17, hakuna timu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyofungwa mabao mengi zaidi kwa penalti kuliko PSG (7) pia ndiyo timu iliyopata penalti nyingi zaidi nyumbani 8.
Mshambuliaji wa PSG, Neymar amekuwa mchezaji wa kwanza kutoka Brazil kufunga mabao mengi katika ligi hiyo amefunga mabao 31 na kupika 19 akimfunika Kaka, aliyefunga mabao 30.
Ushindi dhidi ya Inter Milan wa bao 1-0 haujaisaidia sana Tottenham, licha ya kupanda hadi nafasi ya pili, ikifikisha pointi saba sawa na Inter Milan ina nafasi finyu ya kucheza 16 bora, kwani itaifuata Barcelona katika mechi ya mwisho na ikipoteza inaweza kuangukia Europa Ligi.
Matokeo ya mechi zote za jana Atl Madrid 2 Monaco 0, Borussia Dortmund 0 Club Brugge 0, PSV Eindhoven 1 Barcelona 2, Tottenham 1 Inter Milan 0, Napoli 3 Red Star Belgrade 1, PSG 2 Liverpool 1, FC Porto 3 Schalke 1 na Lokomotiv Moscow 2 Galatasaray 0
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.