Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

2.Ivan Helguera -mabao 16

Mabeki wa Real Madrid wanapenda sana kushambulia na ndio maana pengine wamekuwa wengi kwenye orodha hii kutokana na kufunga mabao mengi kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya. Beki, Ivan Helguera alikichezea kikosi hicho cha Los Blancos kuanzia mwaka 2000 hadi 2007 na hakika alikuwa matata kabisa ndani ya uwanja. Kwenye michuano ya Ulaya alicheza mechi 97 na kufunga mabao 16. Sergio Ramos kazi anayo kuvunja rekodi za mabeki waliomtangulia kwa ufungaji kwenye kikosi hicho.
 
1.Roberto Carlos - mabao 17

Roberto Carlos bado anahesabika kama mmoja wa mabeki wa kushoto bora zaidi waliowahi kutokea kwenye soka duniani. Gwiji huyo wa Brazil alifunga mabao 17 katoka Ligi ya Mabingwa Ulaya katika kipindi chake alichokuwa kwenye kikosi cha Real Madrid na msimu mmoja aliokwenda kuitumikia Inter Milan. Kwenye rekodi zake za ngazi ya klabu alishinda mataji matatu ya Ulaya na manne ya La Liga. Kwenye timu ya taifa ya Brazil amecheza mechi 125 na kufunga mabao 11.
 
Hicho kilikuwa kipigo cha kwanza kikubwa kwa Madrid, bingwa mtetezi wa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, tangu Solari amepewa jukumu hilo la uongozi na bahati pekee waliyonayo ni kwamba waliingia katika mchezo huo wakiwa wameshafuzu hatua ya 16 bora.
 
Katika mchezo huo Fedor Chalov ndiye aliyefungua pazia la mabao katika dakika ya 37 kabla ya Georgi Schennikov kuongeza la pili dakika ya 43 na kwenda mapumziko wakiongoza kwa mabao 2-0.
 
Hata hivyo Real imetinga 16 bora ikiongoza kundi huku AS Roma ikichukua nafasi ya pili licha ya kufungwa 2-1 na Viktoria Plzen ambayo iliweza kujikatia tiketi ya kucheza Europa Ligi, huku CSKA Moscow ikimaliza ya mwisho.
 
Solari aliamua kumtoa Benzema aliyekuwa akipoteza nafasi za kufunga mabao na kumuingiza Gareth Bale mabadiliko ambayo hayakubadili matokeo na kocha huyo alitoka uwanjani akionekana amekasirika.
 
Matokeo yote ya mechi za Ligi hiyo zilizochezwa jana usiku ni, Real Madrid 0 CSKA Moscow 3, Viktoria Plzen 2 Roma 1, Ajax 3 Bayern Munich 3, Benfica 1 AEK Athens 0, Man City 2 Hoffenheim 1, Shakhtar Donetsk 1 Lyon 1, Valencia 2 Man Utd 1 na Young Boys 2 Juventus 1.
 
Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho, amesema kilichosababisha wapoteze mchezo wao dhidi ya Valencia kwenye Uwanja wa Mestalla jana usiku ni bao la kujifunga la beki Phil Jones.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…