Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Pogba aliendelea kuboronga juzi Jumatano katika pambano dhidi ya Valencia akikosa bao la wazi pamoja na kushindwa kutawala dimba. Owen anaamini staa huyo aliyepigwa benchi katika mechi mbili zilizopita kabla ya juzi angekuwa bora kwa makocha wengine.
 
Nakerwa kumtazama kwa sababu najua yeye ni bora kuliko tunavyomuona karibu kila wiki. Niko upande wake kwa sababu sidhani kama jinsi timu inavyocheza au kocha anavyomfundisha inasaidia aupate ubora wake,” alisema Owen.
 
Nadhani kocha inabidi abebe baadhi ya lawama kwa jinsi mfumo wake ulivyo na kwa jinsi anavyomchezesha. Nakumbuka mara ya kwanza aliposaini kulikuwa na viungo wengi waliokuwa wanamzunguka kwa ajili ya kupata ubora wake.
 
Nasikia huruma kwa mtazamo wangu, inakera kumtazama anavyocheza kwa sababu anaonekana kama vile ana umri wa miaka 16 au 17 anajifunza kucheza soka. Nadhani anaweza kujifunza mengi kama ataangalia mikanda ya Paul Scholes. Atajua muda gani wa kupiga pasi moja, muda gani kugusa mpira mara nyingi, muda gani kupiga chenga.
 
Nadhani anachukua uamuzi mbaya katika mechi, kitu ambacho kinakera kwa sababu kama angekuwa anacheza kama anavyopaswa. Kama angekuwa anacheza chini ya Guardiola au Klopp au mtu mwingine wa aina yao nadhani kwa sasa tungekuwa tunamuangalia mmoja kati ya wachezaji bora duniani, lakini kwa sasa hatuwezi kusema hilo.”
 
Balansi ya watu ambao wanamzunguka haijafanya kazi United. Mourinho amejaribu na haijafanya kazi bado. Nadhani pale United lawama zote zinakwenda kwa Pogba au zote zinakwenda kwa Mourinho. Na nadhani ni vigumu sana kulirekebisha hilo. Wanahitaji msaada kwa sababu inaonekana wachezaji wengine wote hawasaidii jambo hili,” alisema Hargreaves.
 
Pogba inabidi ajitume sana. Ana uwezo mkubwa na anafanya hivyo kwa Ufaransa. Inabidi afanye hivyo bila ya kujali kocha ni nani. Inabidi aingie uwanjani na kufanya kazi yake. Hilo ndio jukumu lake,” alisema Mills ambaye pia alivishutumu vyombo vya habari vya Uingereza kwa kuwa na ajenda ya siri na Mourinho.
 
Kinachonishangaza ni wazi kuna ajenda ya siri dhidi ya Mourinho. T

upende tusipende, sana sana katika vyombo vya habari. Unai Emery huwa anasifiwa akimuacha nje Mesut Ozil wanadai amechukua maamuzi ya kishujaa, Mourinho akiwaacha nje Romelu Lukaku na Paul Pogba kwa sababu hawachezi vizuri tunadai ‘huwezi kufanya hivyo kwa mchezaji wako bora’.
 
?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1d6ke4yf980hs.jpg
 
Back
Top Bottom