Nasikia huruma kwa mtazamo wangu, inakera kumtazama anavyocheza kwa sababu anaonekana kama vile ana umri wa miaka 16 au 17 anajifunza kucheza soka. Nadhani anaweza kujifunza mengi kama ataangalia mikanda ya Paul Scholes. Atajua muda gani wa kupiga pasi moja, muda gani kugusa mpira mara nyingi, muda gani kupiga chenga.