Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

ASIKWAMBIE mtu wanasoka wa Kiafrika wamelishika soka la dunia. Huko Ulaya kwa sasa kila kona ni Mohamed Salah. Huko kwenye kikosi cha Arsenal, huwaambii kitu kuhusu Pierre-Emerick Aubameyang kama ilivyo kwa Sadio Mane na Naby Keita kwenye kikosi cha Liverpool na Riyad Mahrez katika chama la Manchester City.
 
Kutokana na umuhimu wao ndio maana wamekuwa wakinaswa kwa pesa nyingi na kuwa miongoni mwa wanasoka ghali kwenye soka la dunia.

Hawa ndio wanasoka sita ghali wa Afrika kwa sasa, wakitamba katika klabu za Ulaya na Mashariki ya Mbali.
 
6. Sadio Mane

- Pauni 35milioni

Mshambuliaji wa kimataifa wa Senegal, Sadio Mane ndiye anayekamata nafasi ya sita kwa wanasoka ghali wa Afrika. Liverpool ilimnasa kwa uhamisho wa Pauni 35 milioni Juni 2016 akitokea Southampton.

Ni mchezaji anayechapa kazi kubwa kwelikweli ndani ya uwanja na hakika amekuwa akifanya mambo makubwa katika kila mechi. Kocha Jurgen Klopp anafahamu vizuri utendaji kazi wa mshambuliaji wake huyo na ndio maana amethubutu hata kumbadilishia namba ya jezi yake akimvisha namba 10 msimu huu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…