Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

ASIKWAMBIE mtu wanasoka wa Kiafrika wamelishika soka la dunia. Huko Ulaya kwa sasa kila kona ni Mohamed Salah. Huko kwenye kikosi cha Arsenal, huwaambii kitu kuhusu Pierre-Emerick Aubameyang kama ilivyo kwa Sadio Mane na Naby Keita kwenye kikosi cha Liverpool na Riyad Mahrez katika chama la Manchester City.
 
ASIKWAMBIE mtu wanasoka wa Kiafrika wamelishika soka la dunia. Huko Ulaya kwa sasa kila kona ni Mohamed Salah. Huko kwenye kikosi cha Arsenal, huwaambii kitu kuhusu Pierre-Emerick Aubameyang kama ilivyo kwa Sadio Mane na Naby Keita kwenye kikosi cha Liverpool na Riyad Mahrez katika chama la Manchester City.
Kweli..
 
Kutokana na umuhimu wao ndio maana wamekuwa wakinaswa kwa pesa nyingi na kuwa miongoni mwa wanasoka ghali kwenye soka la dunia.

Hawa ndio wanasoka sita ghali wa Afrika kwa sasa, wakitamba katika klabu za Ulaya na Mashariki ya Mbali.
 
6. Sadio Mane

- Pauni 35milioni

Mshambuliaji wa kimataifa wa Senegal, Sadio Mane ndiye anayekamata nafasi ya sita kwa wanasoka ghali wa Afrika. Liverpool ilimnasa kwa uhamisho wa Pauni 35 milioni Juni 2016 akitokea Southampton.

Ni mchezaji anayechapa kazi kubwa kwelikweli ndani ya uwanja na hakika amekuwa akifanya mambo makubwa katika kila mechi. Kocha Jurgen Klopp anafahamu vizuri utendaji kazi wa mshambuliaji wake huyo na ndio maana amethubutu hata kumbadilishia namba ya jezi yake akimvisha namba 10 msimu huu.
 
5. Mohamed Salah

- Pauni 36.9milioni

Liverpool iliilipa AS Roma Pauni 36.9 milioni mwaka 2017 kupata saini ya Mohamed Salah. Mmiliki wa AS Roma alisema wakati Liverpool ipo kwenye mazungumzo ya kumsajili Mo Salah mabosi wa timu hiyo walilalamika sana kuuziwa mchezaji huyo bei kubwa, lakini alichokwenda kukifanya kwenye kikosi chao sidhani kama wanaona walimsajili kwa pesa nyingi.

Staa huyo wa kimataifa wa Misri alifunga mabao 32 kwenye Ligi Kuu England na kushinda Kiatu cha Dhahabu, huku akishinda pia tuzo nyingine kibao msimu uliopita. Mo Salah ni mwanasoka ghali namba tano wa Afrika kwa sasa.
 
4. Naby Keita

- Pauni 52.75milioni

Liverpool imekuwa na Waafrika wa maana kwenye kikosi chake kwa sasa. Hakuna ubishi, Kocha Klopp angekuwa kwenye wakati mgumu sana kama michuano ya Afcon ingekuwa ikifanyika kama zaidi kuanzia Januari.

Lakini kwa sasa michuano hiyo imesogezwa mbele na kufanyika kati ya Juni na Julai, hivyo msimu mingine ya ligi inakuwa imekwisha.
 
3.Pierre-Emerick Aubameyang

- Pauni 56milioni

Straika, Pierre-Emerick Aubameyang alikuwa mchezaji wa mwisho kusajiliwa na Kocha Arsene Wenger kabla hajaamua kuachia ngazi kuendelea kuinoa Arsenal baada ya kudumu kwenye timu hiyo kwa miaka 22. Fowadi huyo wa Gabon alitua Emirates akitokea Borussia Dortmund kwa uhamisho ulioigharimu Arsenal Pauni 56 milioni.

Aubameyang ameonyesha uwezo mkubwa wa kufunga mabao ambapo kwa sasa zikiwa zimechezwa mechi 16 tu kwenye Ligi Kuu England tayari staa huyo ameshaweka wavuni mabao 10 na hivyo kuwa kinara wa mabao akilingana na Mohamed Salah.
 
2.Riyad Mahrez

- Pauni 60milioni

Manchester City ilimsajili Riyad Mahrez kutoka Leicester City kwa ada ya Pauni 60 milioni Julai mwaka huu.

Kwa uhamisho huo, staa huyo wa kimataifa wa Algeria sasa amekuwa mwanasoka ghali namba mbili wa Afrika.

Kocha wa Man City, Pep Guardiola alitaka huduma ya Mahrez tangu kwenye dirisha la Januari.

Hata hivyo, kwa wakati huo Leicester City iligoma kumuuza hivyo Mhispaniola huyo alikuja kumpata mchezaji wake anayetaka ilipofika mwisho wa msimu.
 
1.Cedric Bakambu

- Pauni 65milioni

Habari ndiyo hiyo. Mashabiki watasema wanalotaka, lakini ukweli utabaki palepale fowadi wa DR Congo, Cedric Bakambu ndiye mwanasoka ghali zaidi wa Afrika.

Staa huyo alijiunga na klabu ya Beijing Guoan ya China Januari mwaka huu akitokea Sevilla kwa ada ya Pauni 65 milioni. Tangu alipojiunga na timu hiyo amefunga mabao 23 katika mechi 28 akiwa na kikosi chake kipya.

Pesa ndio kivutio pekee kinachowafanya wanasoka kukubali kwenda kucheza soka Ulaya.
 
Back
Top Bottom