Straika, Gabriel Jesus, ambaye alionekana kupoteza buti zake za kufungia msimu huu, mamabo yake yote mawili aliyofunga jana Jumamosi yalitokana na asisti za Mjerumani, Leroy Sane.
Ushindi huo unaleta faraja kwa kocha Pep Guardiola na kuamini kwamba ubingwa bao upo kwenye mipango yao licha ya kutikiswa na Chelsea kwenye mechi iliyopita baada ya kukumbana na kipigo cha mabao 2-0. Liverpool ndio wanaowatisha Man City kwenye mbio za ubingwa kutokana na kuachana pointi chache, lakini Guardiola atakuwa mtu mwenye furaha kama tu mpinzani wake kwenye mbio hizo, Jurgen Klopp atasimamishwa na Jose Mourinho huko Anfield.