Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

.HABARI ndio hiyo. Manchester City hawataki kupoa kwenye Ligi Kuu England na wala hawataki kuwaboa mashabiki wao na ndio maana wanashusha tu vipigo kwa wapinzani wao.
Baada ya kushtushwa na kipigo cha kutoka kwa Chelsea, Man City walirudi kwa kasi kubwa kwenye Ligi Kuu England wakiwachapa Everton 3-1, shukrani kwa mabao ya Gabriel Jesus, aliyetupia kambani zote, moja kipindi cha kwanza na jingine katika kipindi cha pili.
 
Bao la Everton la kujifariji walilofunga kwenye mechi hiyo liliwekwa nyavuni na staa Dominic Calvert-Lewin kwenye kipindi cha pili, dakika chache kabla ya Raheem Sterling kupiga chuma cha tatu kwa upande wa Man City.
Matokeo hayo yanawafanya Man City kurudi kwenye kilele cha msimamo wa Ligi Kuu England, wakikusanya pointi 44, mbili ya waliokuwa vijana kwa wiki moja, Liverpool ambao hii leo Jumapili watakuwa na shughuli pevu ya kuwakabili Manchester United huko Anfield.
 
Straika, Gabriel Jesus, ambaye alionekana kupoteza buti zake za kufungia msimu huu, mamabo yake yote mawili aliyofunga jana Jumamosi yalitokana na asisti za Mjerumani, Leroy Sane.
Ushindi huo unaleta faraja kwa kocha Pep Guardiola na kuamini kwamba ubingwa bao upo kwenye mipango yao licha ya kutikiswa na Chelsea kwenye mechi iliyopita baada ya kukumbana na kipigo cha mabao 2-0. Liverpool ndio wanaowatisha Man City kwenye mbio za ubingwa kutokana na kuachana pointi chache, lakini Guardiola atakuwa mtu mwenye furaha kama tu mpinzani wake kwenye mbio hizo, Jurgen Klopp atasimamishwa na Jose Mourinho huko Anfield.
 
Kasi ya kufunga ya fowadi Sterling imemfanya staa huyo kuzidi kuwapa presha wakali kama Mohamed Salah, Pierre-Emerick Aubameyang na Harry Kane katika mbio za kufukuzia Kiatu cha Dhahabu kwenye ligi hiyo msimu huu.
Mchakamchaka wa ligi hiyo utaendelea leo, ambapo shughuli ya kibabe itakuwa huko Anfield, ambapo Liverpool watamaliza ubishi na mahasimu wao wakubwa, Man United, huku kukiwa na mechi nyingine mbili, ambapo Brighton watawakaribisha Chelsea na Arsenal watakwenda St.Mary's kuwakabili Southampton.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]makoroboi leo hatokei huyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…