Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mwanamke mlemavu amefariki dunia baada ya meno yake yote kung'olewa katika hatua ambayo imekosolewa vikali nchini Uingereza.
Rachel Johnston alifanyiwa oparesheni hiyo baada ya madaktari kubaini kuwa meno yake yote yameoza.
Lakini alizirai saa kadhaa baada ya kutolewa hospitali ambako alikuwa amelazwa kwa siku kadhaa.
 
Familia yake iliyokuwa imejawa na wasisiwasi ilifahamishwa kuwa madaktari hawakuwa na uwezo wa kuyaokoa maisha yake.
Upasuaji huo ulifanywa na wataalamu wa meno katika kituo cha afya cha Worcestershire.
Familia mbili zaidi zimeiambia BBC masaibu yao kuhusu huduma zinazotolewa na kituo hicho zikisema watoto wao wawili wa kiume walifanyiwa upasuaji bila ya wao kufahamishwa.
Katika visa vyote viwili, familia hizo zilitarajia watoto wao waliyokuwa walemavu watatolewa meno kidogo lakini walistaajabu kuwakuta wakiwa wameng'olewa meno yote.
 
Kituo cha afya cha Worcestershire kinashikilia kuwa kinafuata utaratibu uliyofaa kuwahudumia wagonjwa wake japo kuwa mamlaka kadhaa za matibabu nchini Uingereza sasa zinachunguza kifo cha Johnston.
Makundi ya kutetea haki yanasema kuwa kumekuwa na visa vya mgongano wa mawasiliano kati ya wagonjwa wenye ulemavu na familia zao.
Makundi hayo sasa yanatoa wito kwa madktari wa meno kuingilia kati ili kuzuia visa vya mtu kung'olewa meno yote.
"Haifa kabisa kuona hali kama hii ambapo matibabu yanakuwa ya kushtua," alisema said Sarah Coleman, mkaazi wa Mencap.
 
Bi Johnston, 49, amekabiliwa na matatizo ya kuumwa na meno kwa muda hali iliyoifanya familia yake kwenda mbio kumtafutia matibabu.
Mapema mwaka huu familia yake ilifahamishwa kuwa Johnston ''hana budi kung'olewa meno yote''
''Niliuliza kama kuna uwezekano wa binti yangu kung'olwa meno hayo kwa awamu'' anasema mama yake Diana Johnston
Oktoba 26, mwaka huu binti yake ambaye alipata matatizo ya akili baada ya kuugua ugonjwa wa utando wa ubongo akiwa mtoto mdogo alilazwa katika hospitali ya Kidderminster ili kufanyiwa oparesheni ya kung'olewa mena.
 
''Hali ya bi Johnston haikuwa nzuri wakati wa oparesheni hiyo lakini iliimarika'' alisema mama yake.
Siku iliyofuata, maafisa wa hospitali hiyo walimpigia simu na kumfahamisha kuwa binti yake alikuwa anaumwa.
"Alikuwa anatokwa na damu mdomoni na ulimi wake ulikuwa umefura, huku akiwa amelala kama mtu ambaye hana uhai."
Siku iliyofuata alikimbizwa hospitali baada ya kupatikana na matatizo ya kupumua.
Binti yake alilazwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi na baadaye familia ikafahamishwa kuwa madaktari wameshindwa kudhibiti hali yake.
Uchunguzi wa awali umebaini kuwa mgonjwa huyo alifariki siku 10 baada ya mashini kuzimwa.
 
Kuna sababu nyingi zinazofanya meno kuoza ikiwa ni pamoja na kutopiga mswaki, kuongezaka kwa gesi mwilini, na matatizo yanayotokana jeni ya maumbile.
Vituo vya afya ya umma nchini Uingereza hutoa huduma ya kuwaangalia watu waliyo na matatizo ya meno.
Charlotte Waite, mwenyekiti wa chama cha madaktari wa meno nchini Uingereza amesema madaktari lazima wapate idhini ya mgonjwa kumng'oa meno.
 
Ikiwa mgonjwa hana uwezo wakutoa idhini , daktari anaruhusiwa kumpatia matibabu kwa kuzingatia maslahi ya afya yake'' alisema Bi Charlotte.
"Sheria inasema daktari amtibu mgonjwa kwa njia ambayo haitaathiri uhuru wake na kumnyima haki zake za kimsingi."
Wataalamu wanasema si rahisi kumfanyia mgonjwa uchunguzi wa meno bila kumdunga sindano ya kufisha ganzi.
 
Ikiwa mgonjwa hana uwezo wakutoa idhini , daktari anaruhusiwa kumpatia matibabu kwa kuzingatia maslahi ya afya yake'' alisema Bi Charlotte.
"Sheria inasema daktari amtibu mgonjwa kwa njia ambayo haitaathiri uhuru wake na kumnyima haki zake za kimsingi."
Wataalamu wanasema si rahisi kumfanyia mgonjwa uchunguzi wa meno bila kumdunga sindano ya kufisha ganzi.
 
Mahakama ya jeshi nchini Ethiopia imewahukumu wanajeshi 66 kati ya miaka 5 na 14 kwa kuandamana kwenda ikulu ya waziri mkuu Abiy Amhed mwezi Oktoba mwaka huu na kwa kuvunja kanuni za jeshi, kwa mujibu wa maafisa.
Wanajeshi hao 66 walikuwa miongoni mwa wanajeshi 200 waliokuwa wamevaa sare ambao walifika wakiwa wamejihami kwenye majengo ya ikulu ya Abiy tarehe 10 Oktoba katika kile serikali ilisema lilikuwa ni shinikizo na kutaka waongezewe mshahara.
 
Lakini Abiy ambaye alionyeshwa kwenye televisheni akifanya mazoezi na wanajeshi hao alisema viongozi wao walikuwa na nia ya kusitisha mabadiliko nchini humo na wanajeshi ambao hawakutajwa majina walisema walijutia kupoteza fursa ya kumuua Abiy.
 
Kanali Meshesha Areda, mkuu wa mahakama za kijeshi aliwaambia waandishi wa habari kuwa mahakama ya jeshi ilimhukumu mwanajeshi mmoja miaka 14 na wengine 65 kati ya miaka 5 na 13 kwa kukiuka kanuni za jeshi.
 
Hakujakuwa na taarifa kuhusu hatua za kijeshi walizochukuliwa wanajeshi wengine waliokuwa kwenye kundi hilo.
Wakili wa wanajeshi hao Desalegn Dana alisema atakata rufaa kwa washukiwa wachache.
Tangu ateuliwe mwezi Aprili Abiy mwenye miaka 42 ameongoza mabadiliko kadhaa kwenye taifa hilo la Pembe ya Afrika ikiwemo kuwasamehe watoro waliokuwa wamepigwa marufuku na serikali za awali.
 
2 Aprili - anakuwa waziri mkuu baada ya kujiuzulu kwa Hailemariam Desalegn
19 Aprili - anamteua mkuu mpya wa polisi na usalama wa ndani
Mei - awaachilia maelfu ya wafungwa wa kisiasa akiwemo kiongozi wa upinzani Andargachew Tsege
5 Juni - afuta amri ya hali ya hatari miezi miwili kabla
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…