Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ushindi huo ulikuwa wa kulipa kisasi kwani ni timu hiyo ndiyo iliyowatibulia mkakati wa kumaliza bila kupoteza mchezo wowote katika msimu uliopita ilipowafunga mabao 5-4, hivyo Barcelona jana waliingia uwanjani wakidhamiria kulipa kisasi na wakafanikiwa.
 
Hata hivyo Barcelona walilazimika kuvuja jasho kupata ushindi huo kwani hadi dakika 35 timu hizo zilikuwa 0-0, ndipo Messi akafanya vitu vyake kwa kuwalamba chenga mabeki watatu na kupiga krosi iliyomkuta Luis Suárez na kuuzamisha wavuni kirahisi.
 
Baada ya kuingia kwa bao hilo Levante walikuja juu wakitaka kusawazisha bila mafanikio na Messi tena aliwapa maumivu kwa kufunga bao la pili katika dakika ya 43 hivyo Barca kwenda mapumziko wakiongoza kwa mabao 2-0.
 
Messi aliendeleza ubabe wake kwa kufunga mabao mengine mawili katika kipindi cha pili dakika ya 47 na 60 kabla ya kumtengenezea beki Gerald Piqué aliyefunga bao la mwisho dakika ya 88.

Kwa hat trick hiyo Messi amefikisha mabao 50 aliyoyafunga kwa klabu na timu ya Taifa ya Argentina kwa mwaka huu 2018 pekee.
 
Kocha wa Tottenham, Mauricio Pochettino amesema wala hatajali iwapo uongozi utashindwa kumfanikishia usajili katika dirisha la Januari.

Tottenham ilikuwa timu pekee ambayo haikusajili mchezaji yeyote kwa usajili wa kiangazi mwaka huu na wengi waliamini ingefanya vibaya lakini hadi sasa inafanya vema na iko nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu England.
 
Pia, katika usajili wa Januari mwaka huu, Tottenham ilimsajili mchezaji Lucas Moura pekee kutoka PSG ya Ufaransa hivyo kutosajili kiangazi cha mwaka huu kuliwatia hofu mashabiki.

Timu hiyo kwa sasa inakabiliwa na tatizo la wachezaji kutokuwa fiti wakiwemo washambuliaji tegemeo Dele Alli na Harry Kane huku Fernando Llorente akishindwa kuendana na mfumo wa timu.
 
Suala la usajili halitupi presha sana sababu kuna wakati unataka kitu lakini unshindwa kukipata kwa wakati au unakikosa kabisa kwa hiyo hata kama tutashindwa kusajili Januari hamna shida,” alisema.

Kwa mara ya kwanza katika kipindi kirefu Spurs mwaka huu imefanikiwa kuingia hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
 
Back
Top Bottom