Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Unai Emery ameelezwa amekimbia Paris Saint-Germain na kwenda kuinoa Arsenal kwa sababu alishindwa kuwaongoza wachezaji mastaa na wenye hadhi kubwa kama Mbrazili, Neymar.
 
Mchambuzi wa soka huko Ufaransa, Dominique Severac alisema anaamini kocha wa sasa wa PSG, Thomas Tuchel ameweza kuvuna huduma nzuri kutoka kwa Neymar kuliko hata Emery na hilo linatoa tafsiri ya moja kwa moja kwanini Mhispaniola huyo alishindwa kufanya vizuri huko Paris, Ufaransa na kutimkia zake Arsenal, ambako kuna wachezaji wa kiwango cha kawaida tu.
 
Severac alisema Kocha Emery sasa anaonyeshwa na mwenzake Tuchel kile kilichostahili kufanywa kwenye kikosi cha PSG chenye mastaa wa maana kama Neymar, Kylian Mbappe na Edinson Cavani.
 
Emery hajui namna ya kuwanoa mastaa. Na ndio maana yupo kwenye kikosi cha Arsenal. Yeye Emery alikuwa hana mastaa, anamwona Neymar na (Christopher) Nkunku wapo sawa. Ukweli ukiwa Neymar huwezi kuwa na akili za Nkunku. Nkunku mwenyewe pia anafahamu yeye si Neymar na Neymar anafahamu yeye si Nkunku!”
 
UBISHI wa Liverpool na Manchester United ulimalizwa jana Jumapili huko Anfield. Vigogo hao mahasimu walimenyana kwenye mchezo wa Ligi Kuu England na ilikuwa mechi muhimu.
 
Kilichokuwa kikisubiriwa kama kutakuwa na mkali wa kupiga pasi nyingi mchezoni kama walivyowahi kufanya mastaa hawa watano, ambao waliweka rekodi kwa kupiga pasi nyingi kwenye mechi moja ya Ligi Kuu England.
 
Hawa hapa ndio mastaa waliowahi kuweka rekodi ya kupiga pasi nyingi kwenye mchezo mmoja wa Ligi Kuu England huku, Ilkay Gundogan akishikilia rekodi kwa kuongoza kwa pasi kwenye mechi moja ya ligi alipofanya hivyo msimu uliopita dhidi ya Chelsea.
 
5.Santi Cazorla vs Sunderland (2014/15)- Pasi 154

Mashabiki wa Arsenal wanafahamu wazi wangekuwa wanafurahia mambo mengi matamu kwa kumtazama kiungo fundi wa mpira, Santi Cazorla kama si majeraha kumtibulia.

Mwishoni mwa msimu uliopita, Cazorla aliruhusiwa kuondoka kwenye timu hiyo ya Arsenal akienda kujiunga bure kabisa huko Villarreal.

Staa huyo mwenye umri wa miaka 33 anachopambana kwa sasa ni kujaribu kurudisha makali yake kama ilivyokuwa zamani, lakini sasa akiwa huko kwenye La Liga.

Katika msimu wa 2014/15 alikuwa kwenye Ligi Kuu England na hakika alikuwa moto kwelikweli na ndio maana kwenye mechi dhidi ya Sunderland alipiga pasi 154 mchezoni na kuwa miongoni mwa mastaa waliowahi kupiga pasi nyingi katika mchezo mmoja wa Ligi Kuu.
 
4.Yaya Toure vs Stoke City (2011/12)- Pasi 157

Manchester City haina magwiji wengi wenye historia nzuri katika mchezo wa soka kwa mafanikio ya uwanjani.

Lakini tangu klabu hiyo ilipokuwa chini ya Sheikh Monsour kuna mengi yametokea na kila kitu kimekuwa tofauti.

Kiungo Yaya Toure amekuwa mmoja kati ya wanasoka waliofanya vyema na kunufaika na mabilionea hao wa kutoka Mashariki ya Kati.

Toure alitua Etihad akitokea Barcelona na mengine yaliyoendelea hapo yamebaki historia.

Akiwa kwenye ubora wake hasa katika msimu wa 2011/12, Yaya Toure alionyesha makali yake matata kabisa, akiweka rekodi ya kuwa mmoja kati ya wachezaji waliopiga pasi nyingi kwenye mechi moja ya ligi, wakati alipopiga pasi 157 kwenye mechi dhidi ya Stoke City.

Wakati ule ilikuwa rekodi kabla ya kuja kuvunjwa na Ilkay Gundogan, Fernandinho na Jorginho.
 
3.Jorginho vs Newcastle (2018/19)- Pasi 158

Chelsea iliichapa Newcastle United 2-1ugenini kwenye Ligi Kuu England. Mechi hiyo haikuwa na mvuto hadi hapo dakika ya 20 wakati The Blues ilipopata penalti.

Lakini habari kubwa kwenye mechi hiyo haikuwa matokeo, bali ni kile kiwango cha kupiga pasi kilichoonyeshwa na staa mpya wa Chelsea, Jorginho, iliyemsajili kwa Pauni 52 milioni.

Katika mechi hiyo, kiungo huyo Mtaliano alipiga pasi sahihi 158, akikizidi kikosi kizima cha Newcastle, ambacho kilipiga pasi 131 tu kwenye mechi yote.

Kocha Maurizio Sarri alikuwa kwenye wakati mzuri baada ya kuona kiungo wake akiandika rekodi ya kuwa miongoni mwa wachezaji waliopiga pasi nyingi katika mechi moja ya Ligi Kuu England.
 
2.Fernandinho vs Everton (2017/18)- Pasi 164

Pep Guardiola ni fundi wa soka la pasi nyingi. Tangu alipowasili Manchester City, wachezaji wengi kwenye kikosi hicho cha Etihad wameonekana kupandisha viwango vyao vya kiuchezaji.

Mbrazili wao Fernandinho ni mmoja kati yao. Staa huyo amesimama imara kabisa kwenye kiungo ya timu hiyo akihakikisha timu inakuwa na mpira muda wote. Msimu uliopita, kwenye mechi dhidi ya Everton, Fernandinho aliandika jina lake kwenye rekodi tamu baada ya kupiga pasi 164 pekee yake. Pasi zote hizo zilikuwa sahihi.
 
1.Gundogan vs Chelsea (2017/18)- Pasi 167

Mashabiki wa Manchester City hakika hawatakuwa na furaha kutokana na macho ya wengi kumkodolea kiungo Jorginho aliyetua kwenye Ligi Kuu England msimu huu.

Kiungo huyo wa Chelsea, Jorginho alipiga pasi 158 kwenye mechi dhidi ya Newcastle United. Lakini, mashabiki wa Man City wanafahamu wazi msimu uliopita kiungo wao Ilkay Gundogan, alipiga pasi 167 dhidi ya Chelsea.

Hadi kufika sasa, Gundogan ndiye mchezaji aliyepiga pasi nyingi katika mechi moja ya Ligi Kuu England na rekodi yake bado haijafunjwa licha ya wachezaji kupambana kuandika historia zao na kutaka kuivunja rekodi hiyo lakini bado inawatoa jasho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…