Mfungwa apewa masharti ya kuangalia filamu wakati akitumikia kifungo chake jela || . Jangili mmoja nchini Marekani ameamriwa kuangalia filamu ya wanyama ya Bambi kila mwezi baada ya kukutwa na hatia ya kuua “mamia” ya mbawala. Muwindaji huyo kutoka Missouri David Berry Jr anatakiwa kuangalia filamu hiyo walau mara moja kwa mwezi wakati akitumikia kifungo chake cha mwaka mmoja gerezani. Alitiwa nguvuni mwezi Agosti pamoja na ndugu zake wawili kwa kuwaua mbawala, kisha kuwachinja na kuondoka na vichwa huku akiacha miili ya wanyama hao ioze, waendesha mashtaka wamesema. Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Kesi hiyo ni moja ya kesi kubwa zaidi za ujangili kuwahi kuripotiwa kwenye historia ya jimbo la Missouri