Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kocha huyo Mreno ameiacha klabu ikiwa na pointi 19, amekuwa miongoni mwa makocha walioshindwa kuirejesha Man United katika hadhi yake tangu alipostaafu kocha nguli Alex Ferguson, licha ya wadau wa soka kuwa na imani naye.
 
Miongoni mwa makocha wanaopigiwa chapuo la kurithi mikoba ya Jose Mourinho ni Mauricio Pochettino wa Tottenham kwa sasa amekuwa akitajwa mara kwa mara tangu wakati wa kocha Louis van Gaal ambapo mashabiki waliamini Pochettino ndiye angeshika usukani kuliongoza jahazi.
 
Conte ana historia nzuri ya mataji ambapo ana mataji manne ya ligi akiwa na miaka 49 tu, kocha huyu wa zamani wa Juventus na timu ya taifa ya Italia anaweza kuwa na moto kama wa Mourinho jambo ambalo bodi ya timu itapaswa kumuongoza sawasawa.
 
Wengine ni Laurent Blanc aliyeifundisha Paris Saint-German kwa mafanikio makubwa sana na baadaye kupumzika kwa miaka miwili sasa, Leonardo Jardim aliyefukuzwa katika klabu ya Monaco kwa kutofanya vizuri. Wachambuzi wa mambo wanasema hiyo haiwezi kuwa kikwazo kwake kukabidhiwa United.
 
Back
Top Bottom