Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Manchester United imemtangaza aliyekuwa mshambuliaji wake wa zamani raia wa Norway, Ole Gunnar Solskjaer kuwa kaimu kocha mkuu wa klabu hiyo kumrithi Jose Mourinho.
 
Klabu hiyo jana asubuhi ilimfukuza kazi Mourinho baada ya kuiongoza kwa karibu miaka miwili ambapo alianza vizuri lakini baadaye mambo yalibadilika na msimu huu alikuwa katika kipindi kigumu akipata.
 
Taarifa za kuteuliwa kwa Solskjaer, zilithibitishwa na tovuti ya klabu hiyo yenye maskani yake Old Trafford lakini hakukuwa na maelezo yoyote zaidi ya ufafanuzi.
 
Solskjaer mwenye miaka 45, aliifungia Man United mabao 126 katika misimu 11 aliyoitumikia chini ya kocha Sir Alex Ferguson.

Kabla ya kuteuliwa kuinoa Man United, Solskjaer alikuwa akiinoa klabu ya Molde ya nchini Norway kuanzia mwaka 2015 hadi Machi mwaka huu alipojiweka kando lakini akaombwa na kuridhia kusaini mkataba mpya mwanzoni mwa mwezi huu.
 
Waziri Mkuu wa Norway, Erna Solberg, amempongeza nguli huyo wa soka akisema uteuzi wake kuinoa klabu hiyo maarufu duniani kote ni heshima kwa Taifa.

Solskjaer mfungaji wa bao lililoipa Man United taji la Ligi Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich mwaka 1999, mechi yake ya kwanza akiwa kocha itakuwa Jumamosi hii dhidi ya Cardiff City.
 
Iwapo atafanikiwa kufanya vizuri katika mechi atakazoiongoza Man United, pengine akathibitishwa kuwa kocha wa kudumu wa timu hiyo ambayo imepanga kumtangaza kocha wa kudumu baada ya kumalizika kwa msimu huu.

Akiwa mchezaji wa Man United, alitwaa mataji sita ya Ligi Kuu England, mawili ya FA na lile la Ligi ya Mabingwa Ulaya.
 
Anatwaa mikoba hiyo wakati Man United ipo nafasi ya sita katika msimamo ikiwa na pointi 26, ambazo ni 19 nyuma ya vinara Liverpool ambayo Jumapili iliyopita iliwalaza kwa mabao 3-1 ambayo yalichangia kwa kiasi kikubwa kutimuliwa kwa Mourinho.
 
Ugomvi usio na ulazima baina ya Jose Mourinho na wachezaji wake, Paul Pogba, nahodha Antonio Valencia na wengine ndiyo sababu kubwa iliyomfanya atimuliwe na Manchester United hapo jana.

Mbali ya Pogba na Valencia, katika siku za hivi karibuni Mourinho aliwabadilikia kabisa wachezaji waliokuwa vipenzi vyake na kulikuwa na uwezekano mkubwa wangeondoka Januari kama kocha huyo angebaki hao ni Alexis Sanchez, Anthony Martial, Eric Bailly na Luke Shaw.
 
Habari za ndani zinadai kuwa kocha huyo alikosana na wachezaji wengi zaidi ya hao isipokluwa wengi wao hawakutaka kujibizana naye kama walivyofanya akina Pogba.

Ugomvi huo kwa kiasi kikubwa ulichangia timu kufanya vibaya kwa timu na bodi ililitambua hilo ila ilikuwa ikisubiri kupata sababu ya kumtimua, hivyo kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Liverpool, Jumapili iliyopita kikakawa sababu nzuri.
 
Jana baada ya Makamu Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Klabu hiyo, Ed Woodward, kutangaza kutimuliwa kwake Pogba alikuwa wa kwanza kuposti ujumbe wa kufurahia akiposti kwenye mtandao wa Twitter ingawa baadaye kidogo aliufuta.

Waliokuwa wasaizi wake Michael Carrick na Kieran McKenna wamepewa jukumu la kusimamia mazoezi ya leo wakati klabu ikisaka kocha wa muda ambaye pengine akapewa ulaji wa kuiongoza hadi mwisho wa msimu huu.
 
Mourinho ametimuliwa wakati ambapo tayari Paul Pogba aliyemnunua kwa ada iliyovunja rekodi ya Paundi 89 milioni kutoka Juventus mwaka 2016, alishamtuma wakala wake Mino Raiola kuzungumza na Juventus ili aondoke Old Trafford Januari na kurudi zake Turin.
 
Hata hivyo kuna uwezekano mkubwa kuondoka kwa Mourinho kukmafanya kiungo huyo kubadili mawazo na kuamua kubaki Man United.

Hii ni mara ya pili kwa Mourinho kutimuwa ndani ya mwezi huu, baada ya kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Liverpool ikumbukwe alitimuliwa Desemba 17 mwaka 2015 na Chelsea wakati akiinoa kwa mara ya pili, sababu ikiwa ni kipigo na matokeo mabaya kwa ujumla.
 
Tangu kuteuliwa kwake 2016 hadi kuondoka kwake Old Trafford, 2018 Mourinho alikuwa amevuna pointi 176 pekee, wakati mahasimu wao Manchester City ilivuna pointi 222, Tottenham Hotspur pointi 202, Chelsea 200 na Liverpool 196.

Mourinho aliondoka bila hata kuwaaga wachezaji wake ambao wakati akuiondoka walikuwa kwenye uwanaj wa mazoezi wa timu hiyo.
 
Kipigo hicho kiliifanya Man United kuwa nyuma ya vinara wa Ligi hiyo Liver kwa pointi 19, kitu ambacho hakijawahi kutokea katika kipindi cha zaidi ya miaka 27.
 
Gwiji wa soka wa klabu ya Liverpool, Ian Rush ni miongoni mwa mashabiki wengi waliongiwa na hofu baada ya droo ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kuipanga timu hiyo dhidi ya Bayern Munich ya Ujerumani.
 
Rush alisema hofu yake inatokana na rekodi nzuri ya Munich kwa timu za Uingereza katika miaka ya hivi karibuni pamoja na uwingi wa wachezaji wenye uzoefu mkubwa wa mechi za kimataifa na pia namna wanavyoweza kuamua matokeo kwa uwezo binafsi.
 
Timu hizo zilikutana msimu wa mwaka 1970-71, robo fainali Liver ikashinda kwa jumla ya 4-1, msimu wa 1971-72 Kombe la Washindi Bayern ilishinda kwa jumla ya 3-1, 1980-81 nusu fainali ya Washindi Liverpool ilishinda kwa faida ya bao la ugenini baada sare katika mechi zote na 2001 UEFA Super Cup, Liver ilishinda kwa jumla ya 3-2.
 
Timu hizo zilikutana msimu wa mwaka 1970-71, robo fainali Liver ikashinda kwa jumla ya 4-1, msimu wa 1971-72 Kombe la Washindi Bayern ilishinda kwa jumla ya 3-1, 1980-81 nusu fainali ya Washindi Liverpool ilishinda kwa faida ya bao la ugenini baada sare katika mechi zote na 2001 UEFA Super Cup, Liver ilishinda kwa jumla ya 3-2.
 
Hata hivyo alisema anapata matumaini kidogo kutokana na uwepo wa kocha Jurgen Klopp, ambaye sio tu kwamba ameibadili sana Liverpool lakini anaifahamu vizuri Munich.

“Kwa kweli Munich kwetu huo sio nzuri ina rekodi nzuri zaidi yetu hili lina niogopesha ingawa tunaweza kujivunia uwepo wa Klopp na ubora wa washambuliaji wetu Mohamed Salah na Sadio Mane,” alisema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…