Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Chelsea ilishindwa kabisa kujua watumie njia gani kuweza kufunga kwani kila walipolikaribia lango la wapinzani walikuta wakizingirwa na wachezaji kibao hadi kushindwa kufunga ingawa Ross Barkley, Olivier Giroud na Willian walizembea kuzitumia nafasi nzuri walizozipata.
 
Hii timu imenistusha sana kwa kujilinda kwake, muda wote walikuwa langoni kwao ni mashambulizi matano au sita tu waliyoyafanya Bournemouth kwa dakika zote 90, nakumbuka walipiga mashuti mawili tu langoni la Callum Wilson na Lys Mousset yaliyookolewa na kipa wetu Kepa Arrizabalaga,” alisema Sarri.
 
Rekodi

Chelsea imeshinda mechi zote nne za Kombe la Ligi ilizocheza dhidi ya Bournemouth, mbili zikiwa dhidi ya robo fainali.

Mshambuliaji Hazard, ameipatia Chelsea mabao 19 katika michuano mbali mbali msimu huu, akifunga kumi na kupika mengine tisa, ikiwa ni idadi kubwa kuliko mchezaji yeyote wa Ligi Kuu England.
 
Akiuzungumzia mchezo huo kocha msaidizi wa Chelsea, Gianfranco Zola, aliwapongeza wapinzani kwa kuwapa ugumu, akisema waliingia kwenye mchezo huo wakiwatumia wachezaji wa akiba lakini baada ya kuona mambo mazito wakawaingiza Pedro na Hazard ambao waliwapatia ushindi.
 
Back
Top Bottom