Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Beki wa timu ya Vitoria Setubal ya Ureno, Nuno Pinto, amekumbwa na fadhaa baada ya kubainika kuwa na ugonjwa wa kansa.

Beki huyo wa timu ya taifa ya Ureno, amejikatia tamaa ya maisha amepata uungwaji mkono kutoka kwa mashabiki wa soka kote nchini Ureno.
 
Mashabiki walioingia uwanjani kuushuhudia mchezo wa Ligi ya Ureno kati ya Vitoria Setubal na Braga walizimama na kutoa heshima zao kwa mchezaji huyo katika dakika ya 21 ya mchezo huo.

Pinto mwenye miaka 32 katikati ya wiki iliyopita aliungana na wachezaji wenzake, benchi la ufundi na viongozi wa klabu hiyo katika mkutano na waandishi wa habari.
 
Hata Pinto, ambaye maradhi hayo yamefahamika kutokana na kusumbuliwa na pumu alishindwa kuzungumza ikabadi nahodha wa timu hiyo Vasco Fernandes azungumze kwa niaba yake.

“Kwa hakika Pinto amekumbwa na fadhaa, ameogopa sana anajiona kama Dunia imemuelema hata hivyo sisi tunapenda kumtoa wasiwasi yeye na familia yake kuwa tupo naye bega kwa bega, yeye ni katika sisi na hatutaweza kumuach mmoja wetu,” alisema Fernandes.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…