Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

5. Xherdan Shaqiri (Liverpool vs Bayern Munich)

Wakati Shaqiri alipoanza kuliweka jina lake kwenye soka la kimataifa, Bayern Munich ndio klabu yake ya kwanza kubwa kumpatia fursa hiyo ya kutambulika katika pande tofauti za dunia. Februari 9, 2012, klabu yake ya zamani FC Basel ilitangaza Shaqiri amekubali uhamisho wa kwenda kujiunga na Bayern Munich ya Ujerumani kwa ada ya Euro 11.6 milioni.
 
Kwa bahati mbaya, Januari 9, 2015, Shaqiri aliihama Bayern Munich na kwenda kujiunga na Inter Milan kwa ada ya Pauni 15 milioni kabla ya kutua kwenye Ligi Kuu England akianzia Stoke City kabla ya sasa kukipiga kwenye kikosi cha Liverpool. Kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya mtoano ya 16 bora, Liverpool imepangwa kumenyana na Bayern Munich na jambo hilo linamfanya Shaqiri kukutana na waajiri wake wa zamani.
 
4.Mario Mandzukic (Juventus vs At.Madrid)

Katika kipindi chake alichokuwa kwenye kikosi cha Atletico Madrid mwaka 2014, Mario Mandzukic alikuwa tishio kwelikweli na mshambuliaji mkorofi kwa mabeki waliopambana naye.

Baadaye aliamua kuachana na timu hiyo na kwenda kujiunga na mabingwa wa Italia, Juventus mwaka 2015 kwa mkataba wa miaka minne, huku ada yake ikiripotiwa kuwa ni Euro 19 milioni, ambayo ililipwa kwa awamu tatu, huku Euro 2 milioni zikilipwa kulingana na kiwango chake cha uwanjani.

Kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya mtoano ya 16 bora, Juventus imepangwa kumenyana na Atletico Madrid, hivyo jambo hilo litamfanya Mandzukic kwenda kukutana na waajiri wake wa zamani.
 
3.Leroy Sane (Man City vs Schalke 04)

Machi 2014, winga Leroy Sane alisaini mkataba wa miaka mitatu wa kuichezea Schalke 04 ambapo mkataba huo ulikwenda kufika tamati Juni 30, 2017.

Hata hivyo, Mjerumani huyo hakusubiri hadi mkataba wake ufike mwisho akatimkia zake Manchester City ambapo ilimsainisha mkataba wa miaka mitano baada ya uhamisho wake kuripotiwa kugharimia Pauni 37 milioni.

Na sasa, Sane akiwa kwenye kikosi cha Man City kwenye mechi ijayo ya mtoano hatua ya 16 bora kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya timu hiyo itakipiga na Schalke, hivyo itakuwa ni mechi itakayomfanya Sane kukutana na waajiri wake wa zamani. Kinachosubiriwa ni kuona kile ambacho Sane atawafanya waajiri wake hao wa zamani.
 
45977137_267205357245974_6807564874529546898_n.jpg
 
2.Samuel Umtiti (Barcelona vs Lyon)

Hii ni moja ya mechi matata kabisa itakayozikutanisha wachezaji na waajiri wao wa zamani.

Beki wa kati wa Barcelona, Samuel Umtiti aliwahi kuichezea Olympique Lyon na mara ya kwanza kupenya kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo ilikuwa Agosti 16, 2011.

Miaka mitano baadaye, ndipo Mfaransa huyo alipokwenda kujiunga na Barcelona kwa ada ya Euro 25 milioni. Kwenye rekodi zake za kisoka, Umtiti amechezea klabu hizo mbili tu, Lyon na Barcelona na safari hii kwenye mtoano wa Ligi ya Mabingwa Ulaya atakabiliana na waajiri wake wa zamani. Itakuwa ni mechi yenye hisia ya kipekee kwa Umtiti atakaporejea nyumbani kucheza mechi ngumu yenye kutoana kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.
 
1.Angel Di Maria (PSG vs Man United)

Agosti 2014, Angel Di Maria alijiunga na Manchester United kwa ada ya Pauni 59.7 milioni.

Alipotua tu Old Trafford alikabidhiwa jezi namba 7, ambayo huko nyuma ilikuwa ikivaliwa na magwiji tu. Lakini mambo hayakwenda vizuri kabisa kwa staa huyo wa Argentina, alichemsha. Katika mechi 32 alizocheza kwenye kikosi hicho aliishia kufunga mabao manne tu, hivyo akaona inatosha na kuihama Ligi Kuu England. Alipotua Paris Saint-Germain alipandisha kiwango chake na kuwa bora zaidi.

Hivyo safari hii kwenye mtoano wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16 bora, Di Maria atarejea Old Trafford kuwakabili waajiri wake wa zamani na hapo atawaonyesha kama yeye yupo vizuri na hajawahi kuchuja.
 
JOSE Mourinho si kocha tena wa Manchester United.

Baada ya kutua kuinoa klabu hiyo mwaka 2016, Mourinho amejikuta akibaki kwenye timu hiyo yenye maskani yake Old Trafford kwa miaka miwili na nusu tu akifutwa kazi huku mafanikio aliyoacha ni kubeba taji la Europa League na Kombe la Ligi.

Kama ilivyotokea kwenye nyakati zake alizokuwa Chelsea na Real Madrid, mambo ya Mourinho katika timu zake yanatibuka zaidi katika msimu wake wa tatu.
 
Baada ya kuachana na Mreno huyo, mabosi wa Man United wametangaza timu hiyo itakuwa chini ya kocha wa muda hadi mwishoni mwa msimu ndipo watakapohangaika kupata kocha wa kudumu. Kocha wa muda aliyechaguliwa ni gwiji wa timu hiyo, Old Gunnar Solskjaer. Kitu kinachosubiriwa ni kuona ni kocha gani atakayekuja kurithi mikoba ya Mourinho huko Old Trafford kama kocha wa kudumu?
 
Back
Top Bottom