Akielezea namna mtu anatakiwa kutumia pilipili kichaa, Dk. Assey alisema kila kitu kikizidishwa kwenye mwili wa binadamu ni sumu hata kile ambacho ni tiba.
Kula kwa tiba ni kwa kuweka kiasi kidogo kwenye chakula si unaiweka nyingi unawashwa hadi unashindwa kula chakula chenyewe. Kama nilivyosema kila kitu kikizidi kwenye mwili wa binadamu ni tatizo,” alisema.
Ushauri wangu ni kwamba tumia kiasi kidogo cha pilipili kwenye chakula chako, wengine wanapenda kuweka wakati chakula kikiwa jikoni wengine mezani wote wakumbuke kuweka kwa kiasi.”
Mtu anapokula kama kuna sehemu imeziba, pilipili huizibua. Mfano, mtu anapopata mafua makali na kusababisha pua kuziba, ukila pilipili inasaidia kuzibua na unapopiga chafya kitendo kile husaidia kuzibua sehemu iliyoziba na kumfanya mtu aendelee kupumua vizuri,” alisema.
Kadhalika, Dk. Assey alitaja faida zingine za ulaji wa pilipili kichaa kuwa ni kuzuia kuvimba kwa tezi mwilini, kuzuia vidonda vya tumbo na husaidia kupunguza kuenea kwa saratani.
Huondoa maumivu mwilini, huzuia bakteria mwilini, husaidia kuweka sawa uwiano wa tindikali (acid) mwilini, husaidia kuondoa kichefuchefu, kikohozi, homa na ugonjwa wa magoti,” alisema.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.