Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hugo Lloris - bonasi lazima

Kipa namba moja wa Tottenham Hotspur, Hugo Lloris ni staa mwingine aliyeingia kwenye rekodi za kuwa mchezaji aliyeweka mahitaji yake ya ajabu kwenye mkataba wake huko kwenye kikosi hicho cha wababe wa London.

Kwenye mkataba wake huko Spurs, Lloris amehitaji kiwekwe kipengele kinachomruhusu alipwe bonasi kwenye mechi zote za Spurs ambazo amecheza iwe ni sare au hata kama timu imefungwa, lakini yeye chake kiingie kwenye akaunti yake ya benki. Si matakwa ya kiwindewazimu hayo. Lloris anapokea bonasi ya Pauni 3,500 iwe Spurs imefungwa au kutoka sare ilimradi awe tu amecheza mechi hiyo husika.
 
Ezequiel Lavezzi -

nyumba mbili

Staa wa Kiargentina, Lavezzi aliamua kuachana na soka la kiushindani, tena akiihama Paris Saint-Germain na kwenda zake huko China kujiunga na Klabu ya Hebei China Fortune. Unaambiwa hivi, uhamisho huo ulichangiwa zaidi na pesa kwa sababu klabu hiyo ya Kichina ilimpa ofa ya kumlipa mshahara wa maana fowadi huyo. Lakini, kinachoelezwa ni kuwa wakati Lavezzi anakwenda kusaini dili la kuichezea Hebei alitaka timu hiyo kwanza impe nyumba mbili zenye kila kitu, magari mawili, dereva na mpishi binafsi ili akubaliane nao na kusaini kuichezea timu hiyo.
 
Diego Maradona

- ndege binafsi

Diego Armando Maradona alikuwa bonge la staa wakati wa enzi zake wakati anacheza soka. Muargentina huyo anaheshimika kwelikweli. Kwa sasa Maradona ni kocha wa timu ya daraja la pili huko Mexico, Dorados.

Baada ya kustaafu soka kama mchezaji, Maradona aliingia kwenye ukocha na huko amezinoa timu nyingi ikiwamo Al Wasl, ambako anaripotiwa alihitaji apewe ndege binafsi kwenye moja ya masharti yake aliyotoa kwenye kuinoa timu hiyo. Hicho ndicho kinachoripotiwa kuhusu maisha yake na matakwa ya Maradona wakati alipokuwa kwenye kikosi cha Al Wasl.
 
Neymar - hoteli

Paris Saint-Germain ilivunja rekodi ya duniani wakati iliponasa saini ya Mbrazili, Neymar kutoka Barcelona. Staa huyo alitua kwenye kikosi cha mabingwa hao wa Ufaransa kwa ada ya uhamisho ya Euro 222 milioni, ambazo zililipwa kununua mkataba wake huko Nou Camp. Baada ya kutua tu Paris, Neymar akafanywa kuwa mmoja kati ya wanasoka wanaolipwa mishahara mikubwa sana kwa wiki, lakini kinachoelezwa ni kuwa mchezaji huyo alihitaji pia apewe hoteli zaidi ya moja kwenye dili lake hilo la kwenda kuichezea timu hiyo ya Ligue 1 inayomiliwa na matajiri wa Kiarabu.
 
Gervinho

- ufukwe binafsi

Supastaa wa Ivory Coast, Gervinho kwa sasa anakipiga kwenye kikosi cha Parma huko Italia.

Fowadi huyo alishawahi kucheza kwenye vikosi vya Lille, Arsenal na AS Roma kabla ya kwenda huko China kujiunga na Klabu ya Hebei China Fortune na baadaye kurudi zake tena Italia kusaini Parma. Lakini unaambiwa hivi, wakati akiwa huko Hebei China Fortune, staa huyo wa kimataifa wa Ivory Coast alitaka apewe ufukwe binafsi kama moja ya vitu alivyokuwa akitaka apewe na waajiri wake hao na kuelezwa ni moja ya mambo ya kijinga yasiyohusiana kabisa na soka waliyowahi kudaiwa na wachezaji ili wacheze kwenye timu fulani. Gervinho pia alihitaji nyumba kwa ajili ya familia yake pamoja na helikopta.
 
Cristiano Ronaldo -

kuficha siri

Supastaa wa Juventus, Cristiano Ronaldo pengine hakuingia mkataba huo wa kijinga na klabu zake anazochezea, ila fowadi huyo ameripotiwa kusaini vipengele vya siri na wafanyakazi wake binafsi kwa ajili ya kuweka siri ya mambo yake binafsi. Wafanyakazi hao wa Ronaldo hawaruhusiwa kusema chochote kinachohusu maisha binafsi ya Ronaldo na mkataba huo utakwenda kwa miaka 70 baada ya Ronaldo kufariki, hiyo ina maana wafanyakazi hao wa Ronaldo hawaruhusiwi kabisa kuzungumza mambo binafsi ya Ronaldo.
 
Ronaldinho -

wafanyakazi wa ndani

Matakwa ya kijinga yaliyowahi kutakiwa na wanasoka maarufu duniani yalimhusu pia staa wa Kibrazili, Ronaldinho.

Inaripotiwa hivi, fundi huyo wa mpira aliyewahi kutamba sana kwenye kikosi cha Barcelona aliambia Klabu ya Queretaro ya Mexico kuwa impatie nyumba moja matata yenye bwawa la kuogelea, uwanja wa soka la ufukweni pamoja na wafanyakazi wa ndani wanne ambao watakuwa na kazi ya kumhudumia yeye tu anapohitaji huduma akiwa nyumbani kwake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…