Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Wazima humu
gossipcourt-20181230-0002.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
MATUMIZI mabaya ya pesa. Mesut Ozil analipwa Pauni 350,000 kila wiki, lakini wala hazitolei jasho.

Anakula mshahara wa bure. Hivyo ndivyo Arsenal wanavyomlipa Mjerumani huyo kwa wiki. Pauni Laki Tatu na Nusu. Ndio, Pauni 350,000 na hachezeshwi. Kocha Unai Emery ni kama anamwondoa Ozil kwenye kikosi chake.
 
Kila zinapokuja mechi ngumu, Emery anaibuka na kusema Ozil mgonjwa. Ujanja ujanja ambao baadhi ya mashabiki wameushtukia na kumpaka kocha huyo Mhispaniola ampige tu bei kiungo huyo kama hataki kumtumia kuliko kuwadanganya kuwa mgonjwa. Mashabiki wa Arsenal hawaelewi kwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa kuliko wengine wote hachezeshwi kwa sababu zisizoeleweka.
 
Hadi Ijumaa, Ozil alifanya mazoezi na wenzake kwa ajili ya kujiunga na kuwakabili Liverpool, lakini baadaye ikafichuka kwamba jina lake limeondolewa kwa kikosi kwa sababu anaumwa goti. Sawa, majeruhi yamekuwa yakitokea na wachezaji wamekuwa wakikosa mechi kila wiki, lakini hili linaloendelea huko Arsenal, Ozil ana bahati mbaya. Mashabiki hawaelewi kwanini majeruhi ya Ozil yamekuwa yakitokea kwenye mechi kubwa tu. Enzi za Arsene Wenger, sawa Ozil alikuwa akikosa baadhi ya mechi, lakini hilo lisingefanyika kwenye mechi dhidi ya Liverpool.
 
Hii ni mechi ya 13, Ozil akikosa chini ya Emery. Mechi ya jana ilikuwa ya 29 kwa Emery tangu aanze kuinoa Arsenal, ina maana ukitoa mechi 13, Ozil amecheza chini ya kocha huyo Mhispaniola mara 16 tu. Lakini, analipwa Laki Tatu kwa wiki.

“Muuze, usimweke tu benchi,” alisema shabiki mmoja akimzungumzia Ozil baada ya kugundua kwamba hatakuwapo kwenye mechi dhidi ya Liverpool.
 
Emery amekuwa akitoa visingizio vingi kuhusu Ozil, kama si mgonjwa, basi atasema hachezi kwa sababu za kiufundi. Hata hivyo, pengine Emery anaona hana shida nna huduma ya Ozil, kwa sababu hata asipokuwapo, timu imekuwa ikitoa vipigo tu kwa wapinzani. Ozil alikosa mechi ya ushindi wa 3-1 dhidi ya West Ham akidaiwa ni mgonjwa. Alikosa tena mechi dhidi ya Brentford, ambapo Arsenal ilishinda 3-1. Hakucheza dhidi ya Fulham, Arsenal ikishinda 5-1 na hakutumika kwenye mechi dhidi ya Sporting CP na Arsenal walishinda 1-0. Hakucheza pia dhidi ya Blackpool na Arsenal walipiga mtu 2-1 na alikosa mechi nyingine iliyomalizika kwa sare ya bila kufungana dhidi ya Sporting CP kwa madai kwamba amepumzishwa.
 
Ozil alikosa mechi nyingine dhidi ya Bournemouth, ambapo timu yake ilishinda 2-1 na Emery aliongoza timu hiyo kushinda 3-0 dhidi ya Vorskla bila huduma ya Mjerumani huyo. Kipenzi hicho cha mashabiki huyo Emirates, hakucheza pia kwenye mechi ya London derby, ambapo Arsenal waliipiga Tottenham 4-2 kabla ya kukosa mchezo mgumu mwingine dhidi ya Manchester United uliomalizika kwa sare ya 2-2. Haikuishia hapo, Ozil alikosa mechi nyingine dhidi ya Huddersfield Town, ambapo Arsenal walishinda 1-0 na hakucheza dhidi ya Spurs tena kwenye Kombe la Ligi, Arsenal wakichapwa 2-0. Hakucheza mechi ya usiku wa jana na matokeo yake ndio kama ulivyosikia.
 
MATUMIZI mabaya ya pesa. Mesut Ozil analipwa Pauni 350,000 kila wiki, lakini wala hazitolei jasho.

Anakula mshahara wa bure. Hivyo ndivyo Arsenal wanavyomlipa Mjerumani huyo kwa wiki. Pauni Laki Tatu na Nusu. Ndio, Pauni 350,000 na hachezeshwi. Kocha Unai Emery ni kama anamwondoa Ozil kwenye kikosi chake.
 
Back
Top Bottom