Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Simu ambazo haziwezi kutumia WhatsApp na tarehe ya kuacha kutumia
Nokia Symbian S60 baada ya Juni 30, 2017
BlackBerry OS na BlackBerry 10 baada ya Desemba 31, 2017
Windows Phone 8.0 na miundo ya awali Desemba 31, 2017
Nokia S40 baada ya Desemba 31, 2018
Android 2.3.7 na miundo ya awali baada ya Februari 1, 2020
iPhone iOS 7 na miundo ya awali baada ya Februari 1, 2020
 
mambo yanakua kwa haraka sana
 
Simu nyingine zisizotumia WhatsApp
Kufikia Juni mwaka 2017, huduma ya WhatsApp pia ilikuwa imeacha kutumika tena katika aina kadha za simu za zamani zikiwemo zile zilizotumia mfumo wa Windows Phone 7.1, Android 2.1 na Android 2.2, na simu aina ya iPhone 3GS/iOS 6.
Kampuni ya Facebook inayomiliki huduma hiyo ilisema wakati huo kwamba inataka kuangazia kustawisha "huduma katika mifumo inayotumiwa na watu wengi."
 
Kampuni hiyo ilikuwa imeorodhesha simu za BlackBerry OS, BlackBerry 10, Nokia S40 na Nokia Symbian S60 kuwa miongoni mwa simu ambazo zingekatiwa huduma mwishoni mwa mwaka 2016 lakini ikabadilisha uamuzi wake na kuongeza muda hadi Juni 30, 2017.
Simu zilizotumia Android 2.1 na Android 2.2, na simu aina ya iPhone 3GS/iOS 6 hata hivyo zilifungiwa mwishoni mwa 2016.
Hatua hiyo ilikuwa imetangazwa na Facebook mapema mwezi Februari mwaka 2016.
Kampuni hiyo ilijitetea na kusema kwamba haikusudii kuwatupa wateja wake ambao wamechangia sana katika ufanisi wake lakini ni kutokana na mabadiliko ya teknolojia.
"Simu hizi hazina uwezo wa kiteknolojia tunaohitaji kuendelea kuimarisha huduma yetu siku zijazo," kampuni hiyo ilisema.
 
Orodha kamili ya mifumo ya simu ambayo wateja hawawezi kutumia WhatsApp:
Android 2.1 na Android 2.2
Windows Phone 7
iPhone 3GS/iOS 6
BlackBerry OS and BlackBerry 10
Nokia S40
Nokia Symbian S60
Wanaotumia simu zilizofungiwa wameshauriwa kununua simu za kisasa zaidi.
 
maskini Nokia....
 
Ni habari mbaya kwa wale wanaofurahia kile wanachofikiri ni kikombe kimoja cha divai kwa siku.
Utafiti mpya wa kimataifa ulimwenguni uliochapishwa katika jarida la Lancet umethibitisha utafiti uliopita ambao umeonyesha kwamba hakuna kiwango salama cha matumizi ya pombe.
Watafiti wanakubali kwamba unywaji wa kiwango cha kadri unaweza kukulinda dhidi ya ugonjwa ya moyo lakini waligundua kwamba hatari ya saratani na magonjwa huzidi faida yoyote ya pombe mwilini.
Mwandishi wa utafiti alisema matokeo yake yalikuwa muhimu kwa sasa kwa sababu ya mambo mengi yalioangaziwa
 
Je unywaji wa kiwango cha kadri una hatari gani?
Utafiti wa magonjwa ulimwenguni uliangazia kiwango cha matumizi ya pombe na madhara yake ya afya katika nchi 195, ikiwemo Uingereza kati ya 1990 na 2016.
Uchambuzi wa data miongoni mwa watu wenye kati ya umri wa miaka 15 hadi 95, watafiti walitofautisha kati ya watu wasiotumia pombe kabisa na wale ambao hutumia kikombe kimoja cha pombe kwa siku.
Waligundua kwamba kati ya watu 100,000 wasiokunywa pombe, 914 watakuwa na tatizo la afya linalohusiana na pombe ama kupata madhara.
 
Lakini watu wanne zaidi wataathiriwa iwapo watakunywa kikombe kimoja cha pombe kwa siku.
Kwa watu ambao waliokunywa vikombe viwili vya pombe kwa siku, watu 63 zaidi walipata madhara katika kipindi cha ndani ya mwaka mmoja na kwa wale waliokunywa vikombe vitano vya pombe kila siku kulikuwa na watu 338 zaidi waliopata madhara ya kiafya.
Mmoja wa waandishi wa utafiti huo, Profesa Sonia Saxena, mtafiti katika chuo cha Imperial mjini, alisema: "Unywaji wa kikombe kimoja kwa siku unaongeza hatari ndogo lakini ikilinganishwa na idadi kuu ya raia wa London inawakilisha idadi kubwa na kwamba wengi wao hawatumii kikombe kimoja kwa siku.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…