Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mwandishi anayeongoza utafiti huo Dk Max Griswold, katika Taasisi ya Matibabu na Tathmini ya Afya (IHME), Chuo Kikuu cha Washington, alisema: "Uchunguzi uliopita umeonyesha kinga ya pombe kwa hali fulani, lakini tumegundua kwamba hatari za pamoja za kiafya za pombe huongezeka kwa kiasi kwa kutumia kiwango chochote cha pombe.
"Ushirika wa juu kati ya matumizi ya pombe na hatari ya saratani, majeruhi, na magonjwa ya kuambukiza hupunguza madhara ya kinga ya ugonjwa wa moyo katika utafiti wetu.
 
Ingawa hatari za afya zinazohusiana na pombe huanza kuwa ndogo kwa kunywa kikombe kimoja kwa siku, na huongezeka kwa haraka kadri ya watu wanapoendelea kunywa zaidi."
Mnamo mwaka wa 2016, serikali ilipunguza viwango vya pombe ilivyopendekeza kwa wanaume na wanawake kutozidi 14 kwa wiki - sawa na chupa sita za pombe ya wastani au glasi saba zamvinyo
Wakati huohuo, Profesa Dame Sally Davies, afisa mkuu wa matibabu nchini Uingereza, alisema kuwa kiasi chochote cha pombe kinaweza kuongeza hatari ya saratani.
 
'Hatari inayojulikana'
Prof Saxena alisema utafiti huo ulikuwa ni utafiti muhimu zaidi uliofanywa juu ya somo hilo.
Alielezea: "Utafiti huu umepiga hatua zaidi kuliko mwengine kwa kuzingatia mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na mauzo ya pombe, taarifa za kujitegemea juu ya kiasi cha kunywa pombe, kujizuia, data ya utalii, viwango vya biashara haramu na pombe zinazotengezwa nyumbani."
Utafiti huo unaonyesha kwamba wanawake wa Uingereza hunywa vinywaji wastani vya chupa tatu za pombe kwa siku na wameorodheshwa katika nafasi ya nane katika ulimwengu wa watu wanaobugia viwango vya juu vya pombe.
 
Wanaume wa Uingereza kwa kulinganisha, wako katika nafasi ya 62 kati ya nchi 195 zilizofanyiwa utafiti, ingawa pia hunywa wastani wa chupa tatu za pombe kwa siku.
Hii ni kwa sababu viwango vya unywaji pombe vilikuwa vya juu zaidi kwa ujumla kati ya wanaume, na wanaume wa Kiromania hunywa vinywaji zaidi ya nane kila siku.
Kinywaji kilielezewa kuwa na gramu 10 za pombe, ambayo inafanana na glasi ndogo ya divai, chupa ya bia, au whisky.
Kote duniani, mtu mmoja kati ya watu watatu wanakunywa pombe na inahusishwa na vifo vyote kwa wale wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 49.
 
Prof Saxena alisema: "Wengi wetu nchini Uingereza hunywa zaidi ya mipaka salama, na kama utafiti huu unaonyesha hakuna viwango salama.
Mapendekezo yanahitaji kuwafikia watu wengi zaidi na serikali inapaswa kufikiria upya sera yake.
Iwapo unataka kunywa, jifunze mwenyewe kuhusu hatari, na kuchagua hatari unayoijua"
 
Kama haunywi pombe kwasababu za kiafya au unapambana na uraibu hebu fikiria inakuwaje pale unapo lazimishwa kunywa ama kubembelezwa unywe na marafiki au ndugu.
Kipindi hiki cha mwisho wa mwaka kwa jina lengine kinafahamika kama msimu wa Siku Kuu kutokana na kufuatana kwa Siku Kuu za Krismasi na Mwaka Mpya na asilimia kubwa ya wafanyakazi hupendelea kwenda likizo.
Kukutana marafiki ndugu ama familia huu ndio wakati wake. Pombe ni moja kati ya vinywaji ambavyo hutumika zaidi katika mikutano hiyo.
Hata hivyo wapo ambao ni wanyaji sana, wasio kunywa kabisa, wanao jitahidi kuacha pombe, wasio kunywa kwasababu za kiafya huenda wanameza dawa na wapo ambao wanapambana na uraibu yaani adiction hivyo hawatakiwi kuonja pombe.
 
Watu wote hao wanahitaji kujumuika pamoja, lakini changamoto ni pale baadhi ya wanao kunywa pombe wanaona hapana kukaa na mtu asiyekunywa pombe ni kero hivyo lazima wote wanywe.
BBC imezungumza na kijana Isack Mugisha anasema haoni sababu ya kukaa kilabuni na mtu asiye kunywa.
"Unajua unapokuta watu wanakunywa alafu ukaungana nao unaagiza soda aisee inakata stimu bora ukae nyumbani kama unajua haunywi. Raha ya bia wote tunywe afu tuyajenge taratibu hapo aah shwari," anasema Mugisha
Hata hivyo BBC imezungumza na Lomwe yeye anasema huwa anakunywa pombe kakini kwasasa hawezi kunywa pombe sababu anatumia dawa.
"Kwasasa sinywi aisee nimeugua wakati mbaya daah hapa nina dozi ya wiki mbili siwezi kabisa kunywa, washkaji wananiita ila naona bora nisiende maana hata mimi sipendi kukaa na mtu asipokuwa anatupia moto moto. Leo natoka ila wakinilazimisha kunywa pombe sijui itakuwaje ila sita kunywa," anasema Lomwe
 
Mwingereza Matt Haig ambaye ameandika kitabu kilicho uzika sana cha Reasons to stay alive anasema yeye akinywa humletea wasiwasi hofu na uoga anatoa ushauri wa namna ya kufanya ili asinywe pombe.
"hata kama watu hawakulazimishi kunywa nafsi yako tu inajisuta ni kama vile watu wasio kula nyama afu umekaa kati yao unakula unajiona kama unawakosea unaweza ukajiondoa hapo," anasema Haig
 
Anasema ni bora kuto kutoka kwasababu kule utashawishika tu na njianyingine ni kama vile:
Nenda kwenye migahawa na sio Bar
Fanya mazoezi tumia ule muda unaokuwa wazi
Weka wazi kwamba hutumii pombe
Epuka makundi au marafiki wanywaji
Tafuta starehe katika kinywaji mbadala
Badili sehemu ulizokuwa unaenda kupumzika awali na wajulishe watu wako wa karibu
 
Mwingereza Matt Haig ambaye ameandika kitabu kilicho uzika sana cha Reasons to stay alive anasema yeye akinywa humletea wasiwasi hofu na uoga anatoa ushauri wa namna ya kufanya ili asinywe pombe.
"hata kama watu hawakulazimishi kunywa nafsi yako tu inajisuta ni kama vile watu wasio kula nyama afu umekaa kati yao unakula unajiona kama unawakosea unaweza ukajiondoa hapo," anasema Haig
 
Anasema ni bora kuto kutoka kwasababu kule utashawishika tu na njianyingine ni kama vile:
Nenda kwenye migahawa na sio Bar
Fanya mazoezi tumia ule muda unaokuwa wazi
Weka wazi kwamba hutumii pombe
Epuka makundi au marafiki wanywaji
Tafuta starehe katika kinywaji mbadala
Badili sehemu ulizokuwa unaenda kupumzika awali na wajulishe watu wako wa karibu
 
Upweke wa kijamii
Mbali na ukweli kwamba pombe ni sehemu kubwa ama kinywaji kinacho furahiwa katika jamii zetu, utamaduni unabadilika.
Takwimu za hivi karibuni kupitia utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha London unaonyesha theluthi ya vijana wadogo hawanyi pombe kabisa.
Japokuwa vijana wadogo ambao wanasumbuliwa na afya ya akili pia wanatatizo la unywaji pombe kupita kiasi
 
Jennifer Griffin, mtaalamu wa afya ya jamii lakini pia meneja wa taasisi ya huduma ya akili Turn2me anasea watu wanatakiwa kujikita katika kufanya mazoezi kama njia mbadala, lakini pia kuyapa kipaumbele mahitaji binafsi ya msingi.
"Pombe inahusishwa na wasiwasi lakini pia hali ya kukosa raha funaha na kuwa na woga. Lakini kujichanganya ndio namna vijana wadogo hufanya ili kujiunganisha na watu na kutengeneza marafiki. Wasipo jichanganya kwa kuhofia kunywa pombe wanaweza wakaanza kujitenga kisha wakaanza kuteseka na upweke".
Uelewa juu ya athari za kiafya unazidi kukua. Kila mmoja akubali. Mtu anaposema hataki kunywa pombe usimlazimishe wala usimwuulize mara mbili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…