Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Atatua Stamford Bridge na watu wanaamini anaweza kuwa ndiye mrithi sahihi wa supastaa Eden Hazard. Nani huyu mtu?
Mtu huyo jina lake halisi ni Christian Mate Pulisic na alizaliwa Septemba 18, 1998 huko Hershey, Pennsylvania, Marekani. Soka lake la kulipwa alianzia kwenye kikosi cha Burussia Dortmund, lakini kabla ya hapo alicheza kwenye timu nyingine za watoto huko kwao Marekani kabla ya kuwa staa wa maana kwenye mikikimikiki ya Bundesliga. Pulisic anatokea kwenye familia ya wanamichezo na ndio maana imekuwa kitu rahisi kwake kutamba kwenye mchezo wa soka kwa sababu ni kitu kilichopo kwenye damu.
 
Atua Borussia Dortmund, atingisha
Pulisic aliishi England wakati ana umri wa miaka saba na hapo alikuwa akiichezea timu ya watoto ya Brackley Town. Lakini, aliwahi kuishi pia Michigani, ambapo alipata nafasi ya kuichezea Michigan Rush utotoni. Kwa sababu familia yake ilikuwa ikihamahama, basi na yeye maisha yake yakawa ya aina hiyo. Februari 2015, Borussia Dortmund walimsajili, kipindi hicho akiwa na umri wa miaka 16 na walianza kumtumia kwenye kikosi chao cha chini ya umri wa miaka 17.
 
Baada ya kufunga mabao 10 na kuasisti manane katika mechi 15 tu za timu za vijana, Pulisic alipandishwa kwenye timu ya wakubwa kwenye kipindi kama hiki cha mapumziko ya baridi. Baada ya hapo, Pulisic alianza kutumika na mechi yake ya kwanza ya Bundesliga ilikuwa dhidi ya Ingolstadt, Januari 30, 2016, alipoingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Adriann Ramos.
Februari 18, Pulisic alicheza mechi yake ya kwanza kwenye michuano ya Europa League alipoingia kipindi cha pili dhidi ya FC Porto.
 
Mechi yake ya kwanza kuanza kwenye Bundesliga ilikuwa dhidi ya Bayer Leverkusen, lakini alitolewa akaingia Marco Reus. Mechi ya pili kuanza ilikuwa dhidi ya FC Schalke 04, nayo hakumaliza, akatoka kuingia kiungo Ilkay Gundogan. Baada ya hapo, Pulisic akaanza kutingiza kwenye Bundesliga.
 
Acheza mechi 15, apandishwa daraja
Kwenye kikosi cha watoto huko Borussia Dortmund, Pulisic alicheza mechi 15 tu kabla ya kuonekana kuwa na uwezo mkubwa na kupandishwa kwenye kikosi cha wakubwa. Hiyo ilikuwa mwaka 2016 na kipindi hicho alikuwa na umri wa miaka 17. Thamani yake kwenye kikosi ilikuwa kubwa na alihusika kwa kiasi kikubwa wakati Dortmund ilipobeba Kombe la Ujerumani msimu wa 2016-17.
 
Aomba uraia Croatia, achezea Marekani
Pulisic anachezea timu ya taifa ya Marekani na ameshafunga mabao tisa katika mechi 23 alizochezea taifa hilo. Lakini, asili ya Pulisic ni Croatia. Babu yake, Mate Pulisic alizaliwa kwenye kisiwa cha Olib huko Croatia. Wakati anahamia Ujerumani, Pulisic aliomba uraia wa Croatia ili awe anahesabika kama mtu wa kutoka nchi za Umoja wa Ulaya kuepuka kulazimika kuwa na kibali cha kuishi Ujerumani. Jambo hilo lilimfanya Croatia wampe ofa ya kwenda kuichezea timu ya taifa ya nchi hiyo, lakini mwenyewe akakataa na kuamua kuitumikia Marekani kwenye soka la kimataifa.
 
*A New Metal has been added to Chemistry...*

*Name:* Woman
*Symbol:* Wm
*Atomic mass:* Light when first found... tends to get heavier with time.

*PHYSICAL PROPERTIES!!!*
- Boils at any time
- Can freeze at any time
- Melts if treated with love
- Very Bitter if Mishandled

*CHEMICAL PROPERTIES!!!*
- Very Reactive
- Highly Unstable
- Possesses Strong Affinity towards Gold,Silver, Diamond, Platinum, Credit cards, Debit cards & Cheque books
- Money Reducing Agent

*OCCURRENCE!!!*
-Mostly found in front of the Mirror.
-It's highly flammable when mixed with in-laws.
-It has mixed properties when seated with parents.
*# Very harmful to you if she sees you with any element similar to itself!!!* [emoji23]

Please circulate to all scientists

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Aweka rekodi Bundesliga, Chelsea wambeba
Pulisic anashikilia rekodi kibao za Bundesliga na kwenye kikosi cha Dortmund. Yeye ndiye kinda asiyekuwa Mjerumani, ambaye amefunga bao kwenye ligi hiyo, kinda wa kwanza kufunga mabao mawili kwenye Bundesliga, lakini akishika rekodi nyingine ya kuwa kinda wa kwanza kuichezea Dortmund kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya na kufunga bao
 
Huduma hizo matata kabisa ndizo zilizowafanya Chelsea kukubali kutoa mkwanja kunasa saini yake. Pulisic amebebwa na The Blues kwa ada ya Pauni 58 milioni na kwamba ataanza kukipiga kwenye kikosi hicho cha Stamford Bridge kuanzia msimu ujao. Kwa sasa ameachwa akicheza Dortmund kwa mkopo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…