Fabregas ameshinda mataji mawili ya Ligi Kuu England akiwa na kikosi cha Chelsea. Amecheza mechi nyingi kwenye ligi, kuliko Mhispaniola yeyote. Lakini, kwa sasa akijiandaa kuachana na Ligi Kuu England, kuna wachezaji wawili wanaweza kufikia asisti za Fabregas. Mchezaji wa kwanza ni Mhispaniola mwanzake, David Silva. Staa huyo wa Manchester City ana asisti 77 kwenye Ligi Kuu England. Silva, ni Mhispaniola wa pili kucheza mechi nyingi, akicheza 265.
Mchezaji wa pili ni staa wa Liverpool, James Milner mwenye asisti 80.