Mshambuliaji wa Chelsea aliyepo Aston Villa kwa mkopo Tammy Abraham, 21, hakufika kwa kikao cha mazoezi Jumatatu huku taarifa zikidokeza kwamba anakaribia sana kukabidhiwa kwa Wolves. (Mirror)
Marco Silva atawasukuma Everton kununua wachezaji Januari iwapo tu wachezaji ambao amekuwa akiwatafuta kwa muda mrefu watakuwa wanauzwa. (Liverpool Echo)
Meneja wa West Brom Darren Moore anapanga kuzungumza na Wes Hoolahan baadaye wiki hii kuhusu mustakabali wa mchezaji huyo wa miaka 36 kutoka Jamhuri ya Ireland. (Express and Star)
Kiungo wa kati wa Birmingham Luke Maxwell, 21, anatarajiwa kuhamia Solihull Moors kwa mkataba wa kudumu baada ya kukaa nusu ya kwanza ya msimu huu katika klabu hiyo ya Ligi ya Taifa kwa mkopo. (Birmingham Mail)
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.