Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Na hakika Juve nayo imekuwa moto kwelikweli kwenye ligi hiyo ikisaka taji lake la saba mfululizo, huku matamanio yake makubwa ni kubeba ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya. Usajili wa Ronaldo umelenga katika jambo hilo la michuano ya Ulaya.
 
Lakini Don Balon, linadai Ronaldo ana ofa mezani kwake inayosema atalipwa Euro 60 milioni kwa mwaka kama mwisho wa msimu huu atachana na Juventus na kwenda kucheza soka huko Uarabuni.
 
Kinachoelezwa kuna timu moja huko Falme za Kiarabu inataka huduma ya Ronaldo na ipo tayari kulipa mshahara huo matata kabisa. Kwa sasa Ronaldo analipwa Euro 30 milioni kwa mwaka huko kwenye kikosi cha Juventus.
 
.OLE Gunnar Solskjaer anajaribu kuteka akili ya kila mchezaji kwenye kikosi cha Manchester United ili wapambane kwa ajili yake. Kocha huyo wa muda, amekichukua kikosi chake na kwenda nacho huko Dubai kutafuta hali ya joto, huku wakijiandaa na mechi yao ngumu kabisa dhidi ya Tottenham Hotspur Jumapili ijayo.
 
Kwenye mtoko huo wa Dubai, Solskjaer amewaambia wachezaji wake kwamba habanwi mtu, kila mtu afanye anavyojisikia na kuwasisitiza kwamba jukumu la kuitafutia mambo mazuri Man United ni la kila mtu. Jambo hilo limedaiwa kuwafanya wachezaji wa Man United kuona kwamba sasa wanaheshimika na kusimamiwa kama watu wazima.
 
Kwenye mtoko huo wa Dubai, Solskjaer amewaambia wachezaji wake kwamba habanwi mtu, kila mtu afanye anavyojisikia na kuwasisitiza kwamba jukumu la kuitafutia mambo mazuri Man United ni la kila mtu. Jambo hilo limedaiwa kuwafanya wachezaji wa Man United kuona kwamba sasa wanaheshimika na kusimamiwa kama watu wazima.
 
Kwenye ziara hiyo amekosekana mchezaji, Paul Pogba, lakini ataungana na wenzake baada ya siku mbili baada ya yeye kubaki England kufanyiwa matibabu kutokana na maumivu aliyopata kwa kuchezewa rafu na Jonjo Shelvey kwenye mechi dhidi ya Newcastle United. Man United imefikia kwenye hoteli ya One&Only Royal Mirage Arabian Court.
 
Solskjaer amekuwa akisifika kwa kubadili upepo kwenye klabu ya Man United tangu alipochukua mikoba ya kuinoa timu baada ya Jose Mourinho kufutwa kazi.
 
Wachezaji wameambiwa hivi, ratiba ya chai asubuhi ni saa 3, lakini sio lazima, mchezaji anaweza kwenda kupata kifungua kichwa muda wowote anaotaka mwenyewe. Solskjaer amewaambia wachezaji wake hakuna kufanya mambo ya kulazimishana, akifanya hivyo kuangalia akili zao kama watajiweka sana na kujiendeesha kama watu wazima.
 
Mastaa hao wa Man United wameambiwa kwamba kutakuwa na mazoezi magumu siku moja kwa siku na mlo wa mchana itakuwa lazima kwa wachezaji kula pamoja na ule mlo wa usiku, ambapo chakula kitakuwa tayari kuanzia saa 2 usiku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…