Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Pierre-Emerick Aubameyang huko Arsenal hashikiki. Harry Kane ndio usiseme kwenye kikosi cha Tottenham Hotspur na Mohamed Salah kauwasha moto kwenye chama la Liverpool. Romelu Lukaku anakuja upya kwenye kikosi cha Manchester United, akifunga mabao katika mechi tatu zilizopita.
 
Kutokana na hilo, Sarri sasa anataka kushusha pini moja matata kabisa, anamshusha Edinson Cavani huko Stamford Bridge. Ripoti zinadai Chelsea inaisaka kwa nguvu zote huduma ya mshambuliaji huyo wa Paris Saint-Germain, ambaye pia atashawishika kutua kwenye kikosi cha The Blues, kwa sababu huko ataheshimika kama straika namba moja, tofauti na huko Ufaransa, ambapo heshima yake kwa sasa imeshuka tangu timu ilipowanasa mastaa wawili, Kylian Mbappe na Neymar.
 
Cavani akitua kwenye Ligi Kuu England kutafanya mchakamchaka wa vita ya kuwania Kiatu cha Dhahabu kuwa na upinzani mkali kwelikweli.
 
Kwa sasa kwenye ligi, Aubameyang na Kane wanatamba, kila mmoja akiwa amefunga mabao 14, huku Mo Salah akiwa amefunga 13, Aguero 10 na Lukaku amepiga manane. Huo ni mchakamchaka kwenye kuwania tuzo ya ufungaji bora kwenye ligi hiyo. Sarri kwa sasa anatamba na Hazard, mwenye mabao 10, lakini kimsingi staa huyo wa Kibelgiji si mshambuliaji wa kati.
 
Kwenye kikosi cha PSG, Cavani amefunga mabao 10 kwenye Ligue 1 msimu huu na kama Sarri atapata huduma yake, basi atakuwa amekamatia mashine ya mabao na hakika mabeki wa timu pinzani wataisoma ramani.
 
.SUPA Sergio. Wanamwita hivyo, ukiweka kando ile a.k.a yake ya utotoni Sergio ‘Kun’ Aguero. Kwa kifupi tu ni bonge la straika linalobamba huko kwenye mikikimikiki ya Ligi Kuu England akitupia jezi za wababe wa Etihad, Manchester City.
 
Alhamisi iliyopita uwanjani Etihad, Aguero alipiga bonge la bao wakati kikosi chake cha Man City kilipoichapa Liverpool 2-1 na kuzirudisha mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu England kuwa tena na upinzani mkali.
 
Bao lake alilofunga kwenye mechi hiyo limemfanya Aguero kuwa mshambuliaji aliyefunga mabao mengi zaidi kwenye mechi za Big Six tangu kuanzia msimu wa 2011-12. Tangu wakati huo, Aguero amefunga mabao 37.
 
Mastaa wanaomfuatia kwa kufunga mabao mengi kwenye mechi zilizohusisha timu za Big Six tangu msimu wa 2011-12 ni straika Harry Kane, amefunga mabao 21, Wayne Rooney amefunga mabao 20, Robin van Persie amefunga mabao 18 na supastaa wa Chelsea, Eden Hazard amefunga mabao 17.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…