Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

9.Liverpool – wafuasi 67.1 milioni

Pengine Liverpool itatengeneza wafuasi wengi zaidi msimu huu kama itafanikiwa kubeba ubingwa wa Ligi Kuu England. Ilivyo kwa sasa kwenye msimamo wa timu za Ulaya zenye wafuasi wengi kwenye mitandao ya kijamii, Liverpool inashika nafasi ya tisa. Wababe hao wa Anfield, ambao kwenye kikosi chao kuna majembe ya maana kama, Mohamed Salah na Sadio Mane, inafuatiliwa na wafuasi 67.1 milioni kwenye mitandao ya kijamiii.
 
8.Juventus – wafuasi 69.4 milioni

Klabu kubwa kabisa ya Italia, Juventus inashika namba nane kwenye orodha hii ya timu zenye wafuasi wengi kwenye mitandao ya kijamii huko Ulaya, kutokana na miamba hiyo kufuatiliwa na wafuasi karibu 70 milioni. Juventus imeongeza umaarufu wake zaidi baada ya kumsajili supastaa wa Kireno, Cristiano Ronaldo kwenye dirisha lililopita la uhamisho wa majira ya kiangazi mwaka jana. Kwa jumla yake, Juventus inawafuasi 69.4 milioni.
 
7.Man City – wafuasi 72.3 milioni

Pep Guardiola ni mmoja kati ya watu walioifanya Manchester City kuwa na wafuasi wengi kwenye mitandao ya kijamii na kuzizidi klabu maarufu zaidi kama Liverpool. Wababe hao wa Etihad wameripotiwa kuwa na wafuasi 72.3 milioni kwenye mitandao ya kijamiii. Tangu mwaka 2008, wakati timu hiyo ilipochukuliwa na matajiri wa Kiarabu, Man City imeweza kuonyesha upinzani mkali kwenye mbio za ubingwa England na kushiriki mara kwa mara kwenye mikikimikiki ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
 
6.Arsenal – wafuasi 76.2 milioni

Arsenal inashika namba sita kwenye orodha ya klabu maarufu kwenye mitandao ya kijamii ikizizidi Liverpool na Man City. Jambo hilo linamfanya Kocha Unai Emery kufahamu tu ukubwa wa timu anayoinoa na jinsi inavyofuatiliwa huko kwenye mitandao ya kijamii, hivyo timu inapofungwa, basi afahamu wazi kuna kundi kubwa sana la watu wanakuwa wameumizwa. Licha ya kwamba Arsenal haijachukua ubingwa wa ligi kwa miaka mingi, lakini yenyewe ina wafuatia 76.2 milioni kwenye mitandao ya kijamii.
 
5.Bayern Munich – wafuasi 79.2 milioni

Bayern Munich ni moja kati ya timu zilizopo kwenye tano bora ya klabu zinazoongozwa kwa kuwa na kundi kubwa la wafuasi huko kwenye mitandao ya kijamii. Kikosi hicho kinachonolewa na Niko Kovac bila ya shaka ni klabu kubwa kabisa ndani ya Ujerumani na Ulaya kwa ujumla wake kutokana na kuwa na ushiriki mkubwa kwenye michuano mbalimbali. Bayern Munich imekuwa na wafuasi wengi kwenye kurasa zake za Twitter na Facebook, ikiwa na wafuasi wengi kuliko hata Arsenal.
 
4.Chelsea – wafuasi 90.1 milioni

Wababe wa Stamford Bridge, Chelsea ni miongoni mwa timu zenye wafuasi wengi huko kwenye mitandao ya kijamii. Umaarufu wa Chelsea umekuwa mkubwa zaidi tangu klabu hiyo iliponunuliwa na bilionea wa Russia, Roman Abramovich mwaka 2003 na baada ya hapo imefanikiwa kusajili wachezaji wengi wa maana pamoja na makocha maarufu kama Jose Mourinho, Carlo Ancelotti, Rafa Benitez, Guus Hiddink, Felipe Scolari na wengine kibao walioifanya timu hiyo kuwa na wafuasi watapatao 90.1 milioni kwenye mitandao.
 
3.Man United –wafuasi 137 milioni

Hili linathibitisha Manchester United ndio klabu maarufu zaidi Ligi Kuu England ukiweka kando kitendo cha kuwa klabu namba moja iliyofanikiwa zaidi kwenye soka la nchi hiyo. Man United imebeba mataji kibao ya Ligi Kuu England na kikosi chake kimeshuhudia mastaa kibao wakipita kucheza na kuajiri pia makocha mahiri. Man United inashika namba tatu Ulaya kwa kuwa timu inayofuatiliwa zaidi kwenye mitano ya kijamii nyuma ya Barcelona na Real Madrid. Man United ina wafuasi 137 milioni.
 
2.Barcelona – wafuasi 240 milioni

Ukikusanya wafuasi wake kwenye mitandao yake ya kijamii, Barcelona inashika namba mbili kwa kufuatiliwa na wafuasi wapatao 240 milioni. Timu hiyo imepata kutumikiwa na wachezaji mahiri duniani akiwamo Ronaldinho, Lionel Messi, Diego Maradona na Neymar. Wachezaji hao wenyewe tu pekee yao wanatosha kuifanya timu hiyo kuwa maarufu kabla ya kuhesabu mafanikio yao ya uwanja ikiwamo suala la kubeba mataji ya kutosha kwenye michuano mbalimbali ndani na nje.
 
455102571_84235.jpeg
 
kuna swali nimeulizwa kwa makonda nimeshindwa kujibu wa kusaidia nishushie gazet nikopi mie akili imechoka kuzisoma namba

Eti kwanini wengi tunapendelea kuwa anonymous huku JF tofauti na wanaotumia mitandao mingine. Msaada plz niirudie home yangu pendwa
 
Mbali na hilo la usajili, pia Real Madrid kitendo cha kubaba ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya mara nyingi kumeifanya kujiongezea umaarufu wake na ndio maana inaongoza huko Ulaya kwa kufuatiliwa na wafuasi 242.9 milioni kwenye mitandao ya kijamii.
 
Back
Top Bottom