4.Chelsea – wafuasi 90.1 milioni
Wababe wa Stamford Bridge, Chelsea ni miongoni mwa timu zenye wafuasi wengi huko kwenye mitandao ya kijamii. Umaarufu wa Chelsea umekuwa mkubwa zaidi tangu klabu hiyo iliponunuliwa na bilionea wa Russia, Roman Abramovich mwaka 2003 na baada ya hapo imefanikiwa kusajili wachezaji wengi wa maana pamoja na makocha maarufu kama Jose Mourinho, Carlo Ancelotti, Rafa Benitez, Guus Hiddink, Felipe Scolari na wengine kibao walioifanya timu hiyo kuwa na wafuasi watapatao 90.1 milioni kwenye mitandao.