Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Watu watatu wamefikishwa mahakamani nchini Zimbabwe, wakishtakiwa kuiba mkoba uliokuwa na $150,000 (£117,600) pesa taslimu mali ya rais wa zamani wa taifa hilo Robert Mugabe.
Washukiwa hao wa wizi wanadaiwa kutumia pesa hizo kununua magari, nyumba na mifugo.
Jamaa wa rais huyo wa zamani, Constantia Mugabe, ni miongoni mwa walioshtakiwa, kwa mujibu wa taarifa katika vyombo vya habari vya serikali.
Mwanamke huyo anadaiwa kuwa na funguo za nyumba ya kijijini ya Bw Mugabe iliyo eneo la Zvimba karibu na mji mkuu wa Harare, na ndiye aliyewasaidia hao wengine kuingia humo na kufika ulikokuwa mkoba huo.
 
Johanne Mapurisa alinunua gari aina ya Toyota Camry... na nyumba ya $20,000 baada ya kisa hicho," mwendesha mashtaka wa serikali Teveraishe Zinyemba aliambia mahakama ya hakimu eneo la Chinhoyi.
"Saymore Nhetekwa alinunua gari aina ya Honda... na mifugo wengine wakiwemo nguruwe na ng'ombe wa thamani ambayo haijulikani."
 
Bw Mugabe, ambaye kwa sasa ana amiaka 94, aliondolewa madarakani na jeshi la Zimbabwe kwama 2017.
Kufikia wakati wa kufurushwa madarakani, alikuwa amekaa madarakani kwa miaka 37, mwanzoni kama waziri mkuu na baadaye kama rais wa taifa hilo.
Wakati mmoja anakumbukwa kwa kusema kwamba taifa lolote lile haliwezi kufilisika.
 
Dola za Marekani huthaminiwa sana nchini Zimbabwe.
Kimsingi, huwa kuna noti za thamana zinazotolewa na benki ambazo thamani yake hutakiwa kuwa sawa na sarafu hiyo ya Marekani, lakini katika uhalisia huwa thamani yake inachukuliwa kuwa chini kuliko dola zenyewe.
Tangu alipostaafu, Bw Mugabe amekuwa akikabiliwa na matatizo ya kutembea na alikaa miezi kadha Singapore akipokea matibabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…