Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

tapatalk_1546171362947.jpeg
 
FAHAMU KUHUSU " ZIWA NGOZI" NA MAAJABU YAKE..
"ZIWA Ngozi ni moja ya maziwa duniani ambayo yametokana na kulipuka kwa Volicano,ziwa hilo Lililopo Wilaya ya Rugwe Mkoani Mbeya nchini Tanzania katika kijiji cha Mbeye one au mchangani ni la pili kwa ukubwa Afrika.
 
Asili ya jina Ngozi linatokana na jina la kabila la Wasafwa linalomaanisha kitu kikubwa ‘’LIGOSI’’ na ziwa hilo tangu zamani lilikuwa chini ya himaya ya kabila la wasafwa katika koo mbili za machifu ikiwemo ya Chifu Mrotwa Mwalingo (akitawala upande wa magharibi) na chifu Mlotwa Mwalupindi(aliyekuwa akitawala upande wa Mashariki).
 
Ziwa Ngozi lipo usawa wa mita 2600 kutoka usawa wa bahari na limezungukwa na misitu minene ya asili katika safu za milima ya Uporoto na kuna hekari 9,332 ambazo zimetengwa kwajili ya uhifadhi wa eneo hilo.
Ndani ya ziwa Ngozi kuna visiwa viwili vinavyovutia sana kwa muonekano na inatajwa visiwa hivyo hutumika kwajili ya mazalia ya bata pori na ndege wengine.
 
Ziwa hilo lina kina cha mita 74 na urefu wa kilometa 2.5 pamoja na upana wa kilometa 1.5 na eneo lake ni km za eneo 3, na pembezoni mwa ziwa hilo kuna mabonde makubwa yenye misitu mikubwa ya miti ya asili na baadhi ya mimea hiyo ni migomba ya asili na mianzi ya asili pamoja na miti mirefu na maua ya aina mbalimbali.
 
Back
Top Bottom