Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

.HII inaitwa mwenye kupata apate. Arsenal bado inakaza kwenye mpango wake wa kumnasa staa wa Barcelona, Denis Suarez kwenye dirisha hili la Januari, lakini katikati ya mpango huo kuna Chelsea nayo imejipenyeza.
 
Kocha Unai Emery ameweka wazi anamtaka mchezaji huyo kwenye kikosi chake, hata kama ni kwa mkopo. Lakini, Barcelona nayo inasema haitaki Suarez aondoke kwenye dirisha hili la Januari.
 
Hata hivyo, kila kitu kinaweza kuwa tofauti ndani ya dirisha hili la Januari kama tu Barcelona itapata mshambuliaji inayemhitaji katika kipindi hiki cha usajili wa majira ya baridi huko Ulaya. Kwenye orodha ya washambuliaji inayowataka Barcelona, mmoja wao ni Alvaro Morata wa Chelsea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…