Fulham, Huddersfield na Leeds ni miongoni mwa vilabu vilivyo na hamu ya kumsajili mchezaji wa Columbus Crew na timu ya taifa ya Marekani Gyasi Zardes, aliye na miaka 27. (Teamtalk)
Leeds pia inapanga kumwania winga wa Wales Daniel James, aliye na miaka 21, na winga wa Ecuador Jefferson Montero, mwenye miaka 29, ambao wote wanaichezea timu ya Swansea.(Sun via Wales Online)
Manchester United inamtaka mlinzi wa Uholanzi Timothy Fosu-Mensah asalie kwa mkopo Fulham lakini timu hiyo inataka mchezaji huyo wa miaka 21 aondoke ili ipokee wachezaji zaidi kwa mkopo. (Sun
Aliyekuwa mchezaji wa Manchester United Andy Cole anatarajiwa kujiunga na Sol Campbell huko mjini Macclesfield kama kocha wa washambuliaji wa timu hiyo. (Mail)
Manchester United wanatafakari uwezekano wa kumuajiri meneja wa timu ya taifa ya England Gareth Southgate huku kampeini ya kumtafuta mrithi wa Jose Mourinho ikiendelea. (Sunday Telegraph)
Meneja wa Atletico Madrid Diego Simeone, ambaye mkataba wake na klabu hiyo ya Uhispania unakamilika miezi 18 ijayo pia yuko katika orodha ya meneja mpya wa United. (Sunday Mirror)
If the bride's parents dance a lot on the
wedding day...my brother just know she has a baby you don't know about
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787]
Don't argue with me, I'm speaking from experience[emoji38][emoji38][emoji38]
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.