.KIUNGO wa Kibrazili, Philippe Coutinho anataka maelezo kutoka kwenye Bodi ya Wakurugenzi wa Barcelona kutokana na namna anavyofanyiwa na kocha wa timu hiyo, Ernesto Valverde.
Kwa sasa kwenye kikosi cha Barcelona, Coutinho amekuwa akijikuta akiwekwa benchi huko Ousmane Dembele akipewa nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza jambo ambalo linamvuruga Mbrazili huyo kwa sasa.
Coutinho licha ya kufunga kwenye mechi ya kipigo kutoka kwa Levante kwenye Copa del Rey, staa huyo wa zamani wa Liverpool alikosolewa na Kocha Valverde kuhusu uchezaji wake.
Siku za karibuni, Coutinho amekuwa akiripotiwa kuwekwa kwenye orodha ya wachezaji wa kupigwa bei na Barcelona huku Man United ikihusishwa na mpango wa kunasa.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.