Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

REAL Madrid imeweka mkakati kabambe kabisa wa kuvamia kwenye Ligi Kuu England na kuchota viungo wawili matata wa kushambulia ili kukifanya kikosi chake kuwa tishio huko Santiago Bernabeu.
 
Ripoti kutoka England zinadai, Los Blancos wanapiga hesabu za kumnasa staa wa Chelsea, Eden Hazard na supastaa wa Tottenham Hotspur, Christian Eriksen.
 
Mastaa hao wawili matata kabisa kwenye Ligi Kuu England wamewekwa kwenye rada za Real Madrid ili kwenda kuifanya kuwa tishio kwenye La Liga na Ligi ya Mabingwa Ulaya.
 
Ofa yake kwa kila mchezaji itaanzia Pauni 50 milioni, huku mabingwa hao wa Ulaya wakiamini kuwa lazima tu ofa zao za kwanza zitagomewa, lakini wataendelea na mchakato wao wa kuwanasa wakali hao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…