Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Wachezaji wote hao mikataba yao itafika tamati mwishoni mwa msimu ujao, hivyo Spurs na Chelsea zipo kwenye hatari ya kuwapoteza mastaa wao kwa pesa kiduchu kama watashindwa kuwasainisha mikataba mipya.
 
Real Madrid jana Jumapili ilitarajia kuifuata Real Betis kwenye mchezo wa La Liga, huku mabingwa hao mara 13 wa Ulaya wakiwa wameachwa pointi kibao na mahasimu wao vinara, Barcelona.
 
. Kocha wa muda wa Ole Gunnar Solskjaer amesema kipa David de Gea amethibisha mwenyewe kuwa ni moja ya makipa bora waliowahi kutokea Manchester United.
 
Katika miaka yake 11, aliyokuwa mshambuliaji ndani ya Old Trafford, Solskjaer alicheza pamoja na makipa bora Edwin van der Sar na Peter Schmeichel.
 
Tumekuwa na rekodi ya kuwa na makipa bora katika klabu hii nafikiri anaweza kulinganana na Edwin na Peter katika orodha ya makipa bora katika historia ya klabu hii," alisema Solskjaer.
 
De Gea aliokoa mashuti 11 yaliyokuwa yanaelekea golini ikiwa ni idadi kubwa zaidi kuwahi kutokea katika Ligi Kuu England huku akiendelea kulinda rekodi ya kutoruhusu wavu wake usiguswe na kuiongoza Man United kushinda mechi sita kati ya sita waliozkuwa chini ya Solskjaer.
 
Mhispania huyo alijiunga na Man United akitokea Atletico Madrid mwaka 2011 tangu wakati huo amefanikiwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa klabu hiyo mara nne katika misimu mitano iliyopita.
 
Ushindi huo wa tano mfululizo wa Ligi Kuu chini ya Solskjaer inafanya Man United inayoshika nafasi ya sita kuwa sawa kwa pointi na Arsenal inayoshika nafasi ya tano, huku wakiwa nyuma kwa pointi sita kuingia katika nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…