Gabriel Jesus alifunga mabao mawili na kuwawezesha Manchester City kuwalaza Wolves mabao 3-0 na kupunguza uongozi wa Liverpool kileleni hadi alama nne.
City hawakuweza kurejelea ufungaji wa mabao mengi ambao walikuwa wameandikisha dhidi ya Rotherham (7-0) na Burton (9-0), ambapo kwa jumla walikuwa wamefunga mabao 16.
Lakini si wengi walikuwa na shaka kwamba wangeibuka washindi, ingawa kwa mabao machache. Hata hivyo, wapo waliotarajia Wolves watoe ushindani mkali ikizingatiwa kwamba wamekuwa mwiba kwa klabu kubwa.
Jesus alianza ufungaji wa mabao dakika ya 10 pale Leroy Sane alipoifikia pasi kutoka kwa Aymeric Laporte na akamwandalia Mbrazil huyo mpira safi na kumuwezesha kufunga.Gabriel Jesus alifunga mabao mawili na kuwawezesha Manchester City kuwalaza Wolves mabao 3-0 na kupunguza uongozi wa Liverpool kileleni hadi alama nne.
City hawakuweza kurejelea ufungaji wa mabao mengi ambao walikuwa wameandikisha dhidi ya Rotherham (7-0) na Burton (9-0), ambapo kwa jumla walikuwa wamefunga mabao 16.
Lakini si wengi walikuwa na shaka kwamba wangeibuka washindi, ingawa kwa mabao machache. Hata hivyo, wapo waliotarajia Wolves watoe ushindani mkali ikizingatiwa kwamba wamekuwa mwiba kwa klabu kubwa.
Jesus alianza ufungaji wa mabao dakika ya 10 pale Leroy Sane alipoifikia pasi kutoka kwa Aymeric Laporte na akamwandalia Mbrazil huyo mpira safi na kumuwezesha kufunga.