Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Liverpool, Tottenham na Everton ni miongoni mwa vilabu katika ligi ya England walio na hamu ya kusmajili winga wa Uholanzi Arnaut Danjuma Groeneveld, aliye na miaka 21, kutoka Club Brugge. (Mail)
 
Juventus na AC Milan itafanya mazungumzo kuhusu azma ya mshambuliaji mwenye miaka 31 Gonzalo Higuain kutaka kujiunga na Chelsea. Mchezaji huyo amechukuliwa kwa mkopo na Milan kutoka timu bingwa katika Serie A, Juve. (Evening Standard)
 
Mabingwa wa Ligue 1 Paris St-Germain wanahitaji mchezaji wa kiungo cha kati mlinzi na wanamlenga mchezaji wa Everton na timu ya taifa ya Senegal Idrissa Gueye, mwenye umri wa miaka 29. (L'Equipe)
 
West Ham imeanzisha mazungumzo kuhusu kumsajili mlinzi anayepigiwa upatu wa Bristol Rovers Michael Kelly, aliye na miaka 21. Mkataba wa mchezaji huyo wa Uskotchi unamalizika mwishoni mwa msimu. (Football Insider)
 
Everton inajitayarisha kumhamisha mshambuliaji raia wa Uhispania anayeichezea Espanyol Borja Iglesias, mwenye miaka 25, aliye na kifungu cha thamani ya £25m katika mkataba wake kuruhusu kuuzwa. (Sun)
 
Marseille bado ina hamu ya kumsajili aliyekuwa mshambuliaji wa Nice Mario Balotelli, mwenye miaka 28, lakini wameshindwa kukubaliana mshahara na mchezaji huyo wa zamani wa Manchester City. (L'Equipe)
 
Uhariri katika gazeti la Uhispania Marca umemshauri mchezaji wa kiungo cha kati wa Real Madrid Isco kuwabadili wawakilishi wake katika vyombo vya habari au ahatarishe kuiangamiza taaluma yake Bournemouth. (Marca)
 
22402a8b-a30b-4655-a90a-dc6f47e99646.jpeg
 
Back
Top Bottom