Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

It's like I know her
2016-09-13%2012.30.31%201338310211530561812_3662913405.jpeg
 
Kipa wa Arsenal ametangaza kustaafu mwishoni mwa msimu huu baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa mafanikio tangu mwaka 2015.

Kipa huyo mwenye miaka 36 alijiunga na Arsenal tangu Juni mwaka 2015 akitokea klabu pinzani ya Jiji la London, Chelsea ambako aliitumikia kwa miaka 11.
 
Cech alizua sinfahamu Oktoba mwaka 2006 baada ya kupata majeraha na kuhitajika kufanyiwa matibabu kutokana na kupasuka kutokana na kugongana na mchezaji wa Reading, Stephen Hunt.

Alilazimika kuwa nje ya uwanja kwa miezi mitatu na tangu hapo akawa anavaa kifaa cha kujilinda sehemu ya kichwa.
 
Solskjaer ambaye ni staa wa zamani wa timu hiyo ameiwezesha United kushinda mechi tano mfululizo za Ligi Kuu ya England na kujikusanyia pointi 15 tangu alipokalia kiti hicho.

Wafuatao ni makocha wengine ambao waliitendea haki nafasi hiyo ya kocha wa muda.
 
Joe Kinnear (Newcastle, mechi 14 Pointi 18)

Aliposhika nafasi ya muda katika uwanja wa St James’s Park pale Newcastle alihakikisha kuwa mashabiki waliona mabadiliko haraka iwezekanavyo.

Alikuwa amechukua nafasi hiyo kuziba pengo la kocha, Kevin Keegan Septemba 2008.

Alianza kwa sare mbili mfululizo kabla ya kuwafokea waandishi wa habari na kugoma kuongea nao tena. Baadaye akashinda mechi mbili mfululizo dhidi ya West Brom na Aston Villa ambazo ziliisaidia timu yake kuondoka katika maeneo ya hatari ya kushuka daraja.

Tajiri wa timu, Mike Ashley aliamua kumpa kibarua cha kudumu baada ya miezi miwili tu lakini miezi mitatu baadaye akaachia ngazi baada ya kuwa mgonjwa. Kwa ujumla alichota pointi 14 katika mechi 18.
 
Guus Hiddink (Chelsea, mechi 13 pointi 34)

Kocha mkongwe wa Kidachi ambaye alionekana kuwa suluhisho kubwa la matatizo ya Chelsea pindi wanapofukuza makocha wao. Tajiri, Roman Abramovich aliweka imani kubwa juu yake lilipokuja suala la kuokoa jahazi kwa muda.

Mara ya kwanza kuitwa kuokoa jahazi ilikuwa Februari 2009 wakati Abramovich alipomfukuza kocha wa Kibrazil, Luiz Felipe Scolari. Hiddink alijikuta akiifundisha Chelsea huku pia akiendelea na kazi yake ya kuwa kocha mkuu wa Russia.

Aliiwezesha Russia kutinga nusu fainali ya Euro 2008 lakini hapo hapo alikuwa tishio akiwa na Chelsea ambapo alishinda mechi 11 kati ya 13 za Ligi. Vile vile alichukua taji la FA. Desemba 2015 alirudi tena klabuni hapo kuchukua nafasi ya Jose Mourinho ambaye alifukuzwa.

Alicheza mechi 12 bila ya kupoteza. Ilikuwa ni rekodi kwa Ligi Kuu ya England kwa kocha mpya kucheza mechi 12 bila ya kufungwa. Kwa ujumla alikusanya pointi 34 katika mechi 13 kama kocha wa muda. Alipendelea zaidi kuwa kocha wa muda, hakuwahi kutaka kuwa kocha wa kudumu.
 
Roberto Di Matteo (Chelsea, Mechi 12 Pointi 24)

Alikuwa kocha msaidizi wa kocha wa KIreno, André Villas-Boas kwa zaidi ya mwaka.

baadaye kocha huyo wa Kireno alitimuliwa na kazi ikaenda kwa Di Matteo ambaye ni staa wa zamani wa timu hiyo. Ilikuwa mnamo Machi mwaka 2012.

Muitaliano huyu alifanya mabadiliko kwa haraka. Wakati akichukua timu Chelsea walikuwa nje ya Top Four na pia walikuwa wamepigwa mabao 3-1 katika pambano la kwanza la Ligi ya Mabingwa hatua ya mtoano dhidi ya Napoli ya Italia.

Di Matteo aliwageuzia kibao Napoli na moja kwa moja akaenda mpaka fainali ambapo aliipa Chelsea ubingwa wa kwanza wa Ligi ya mabingwa kwa ushindi wa matuta dhidi ya Bayern Munich.
 
Kwa kufanya hivyo Chelsea ilikuwa klabu ya kwanza London kutwaa ubingwa wa Ulaya. Lakini katika Ligi alichukua wastani wa pointi mbili katika kila mechi mpaka mwisho wa msimu.

Baadaye Di Matteo alichukua taji la FA na moja kwa moja alikuwa amemshawishi vya kutosha tajiri Roman Abramovich ampe kibarua cha kudumu. Alipewa kibarua cha kudumu lakini msimu uliofuata mambo yalikwenda ovyo na akafukuzwa Novemba.
 
Rafael Benítez (Chelsea, mechi 26 pointi 51)

Kuondoka kwa Di Matteo ghafla ghafla kuliifanya Chelsea iingie katika kibarua ilichozoea cha kutafuta kocha wa muda.

Kwa mshangao wa wengi, hasa mashabiki wa timu hiyo, kazi hiyo ilikwenda kwa kocha anayeheshimika zaidi Liverpool, Rafa Benitez.

Mashabiki hawakumpenda Rafa kutokana na kauli alizotoa dhidi yao wakati akiwa kocha wa Liverpool. katika mechi ya kwanza tu Benitez alizomewa na baadhi ya mashabiki wa chelsea.
 
Garry Monk (Swansea, mechi 14 pointi 18)

KOCHA wa kiingereza ambaye alianza katika mchezo wa kuteleza katika barafu na kujikuta akiangukia katika mchezo wa soka.

Mechi yake ya kwanza baada ya kuchukua timu kwa muda kutoka kwa kocha wa Denmark, Michael Laudrup Swansea City ilikuwa dhidi ya Cardiff City na walishinda.

Wakati huo hali ilikuwa mbaya kwa Swansea lakini Monk aliiwezesha Swansea kutoshuka daraja huku ikiwa na mechi moja mkononi. Kazi yake nzuri ilimuwezesha kupewa kibarua cha kudumu na msimu ujao aliiweka timu katika nafasi ya nane. Hata hivyo alifukuzwa kazi msimu mwingine uliofuata mnamo Desemba 2015 baada ya Swansea kuchemsha katika Ligi huku akishinda mechi moja tu katika mechi 11.
 
Tim Sherwood (Tottenham)

Staa huyu wa zamani wa Tottenham na timu ya taifa ya England alichaguliwa kuwa kocha wa muda wa Tottenham baada ya kuondoka kwa Andre Villas-Boas mwaka 2013.

Sherwood, ambaye awali alikuwa kocha wa vijana chini ya umri wa miaka 21 aliichukua timu ambayo ilikuwa inashika nafasi ya 17 na kufanya mabadiliko makubwa. Aliimarisha kwa kuwapa nafasi makinda kama Nabil Bentaleb na mwisho timu ilishika nafasi ya sita.

Hata hivyo mwisho wa msimu Sherwood alifukuzwa na bosi wa Spurs, Daniel Levy kutokana na timu kushindwa kuingia Top Four. Msimu uliofuata alikwenda kuinoa Aston Villa.
 
UNAAMBIWA hivi, kama kuna kipindi kigumu zaidi kilichowahi kuwakabili Manchester United katika uteuzi wa kocha mpya tangu alipoondoka Sir, Alex Ferguson basi ni kipindi hiki cha sasa cha kuelekea mwisho wa msimu.
 
Back
Top Bottom