Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Calderon alisema uamuzi wa Perez wa kumpiga bei Cristiano Ronaldo uliopangwa mapema ulimtibua Zidane na kuamua kuachana na timu hiyo. Zidane na Ronaldo wote waliachana na timu hiyo ya Bernabeu majira ya kiangazi mwaka jana, kocha akiachia ngazi na mchezaji akiuzwa kwenda Juventus.
 
Calderon, ambaye alikuwa rais wa Madrid kati ya mwaka 2006 na 2009 alisema yote hayo kayataka Perez kwa uamuzi wake wa kumuuza Ronaldo na kumwaacha Gareth Bale kwenye kikosi kitu ambacho Zidane hakukitaka kabisa.
 
Zidane alisisitiza kumbakiza Cristiano na Bale ndio auzwe,” alisema Calderon na kuongeza. “Lakini, Perez amefanya kinyume chake. Zidane alitaka kuwa mtu mwenye kuwa na uamuzi kwenye timu juu ya nani asajiliwe na nani auzwe, lakini hilo lilishindakana, akaamua kuondoka. Ulikuwa uamuzi sahihi.”
 
Ripoti za kutoka Nou Camp zinadai Barca inaweza kukubali kumpiga bei staa huyo aliyemnasa kwa Pauni 142 milioni Januari mwaka jana tu hapo, ili wachangishe pesa ambazo zitatosha kufanya usajili mwingine wa maana, ikiwamo wa kumrudisha Neymar kwenye chama lao.
 
Ugumu uliopo Coutinho ambaye amekuwa akiwekwa benchi na Kocha Ernesto Valverde anataka kupambana na kupata namba kwenye kikosi hicho baada ya kuona Ousmane Dembele akipewa nafasi zaidi. Wakati anatua Nou Camp, Coutinho alisema amejiunga kwenye timu ya ndoto zake, hivyo suala la kukubali kuondoka kwenye timu hiyo kirahisi litakuwa gumu. Lakini kuna kitu kinaitwa pesa, ambacho kinaweza kubadili sura ya mchezo muda wowote ule.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…