Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 348,970
- 1,252,247
Kwenye dirisha lijalo la majira ya kiangazi, chochote kinaweza kutokea na kama Barcelona itafungua milango, basi Man United inaweza kufanya mchakato wa kumbeba Mbrazili huyo, aliyewahi kuwatumikia mahasimu wao wa Ligi Kuu England, Liverpool. Kwenye dirisha lijalo la usajili huko Ulaya, Man United ina sura za mastaa wengi inaohitaji kuwaingiza kwenye kikosi chake licha ya kwamba jambo hilo linaweza kuwasababisha pia kupoteza baadhi ya wakali wake akiwamo Alexis Sanchez na Paul Pogba.