Ripoti zinadai Man United inataka kupunguza bili ya mishahara kwenye kikosi chake na hilo linaweza kuifanya ikubali kirahisi kuwafungulia mlango wa kutokea Sanchez na Pogba, huku ikilenga kwenye kuwakamata mastaa kama Douglas Costa na Coutinho. Wachezaji wengine inayowataka Man United, ambao haitavunja benki yake kwenye kuwalipa mishahara kila wiki ni mabeki Eder Militao, Kalidou Koulibaly na Toby Alderweireld, huku kwenye kiungo ni Douglas Costa, James Rodriguez, Adrien Rabiot, Coutinho na Axel Witsel.