Ripoti zinadai Arsenal inataka kulipa Pauni 1.7 milioni ili kumchukua Suarez kwa mkopo kwanza kwa makubaliano ya kulipa Pauni 17.5 milioni mwishoni mwa msimu ili kumbeba jumla mchezaji huyo.
Dili hilo bado halijakamilika na kinachoonekana ni Arsenal yenyewe tu ndio inayojichelewesha, lakini mchezaji mwenyewe yupo tayari kwenda kuungana na wenzake kufanya kweli kwenye mchakamchaka wa kuhakikisha timu hiyo inamaliza msimu ikiwa ndani ya Top Four.
Suarez amejiona tayari kama ameshatua Arsenal baada ya kushindwa kuficha mapenzi yake wakati alipoonekana kama vile ameungana na Washika Bunduki hao kushangilia ushindi waliopata mbele ya Chelsea kwenye Ligi Kuu England juzi Jumamosi.
Ligi Kuu England ilituma picha za wafungaji hao wa mabao ya Arsenal kwenye ukurasa wake wa Instagram na Suarez hakutaka kujivunga na kubonyeza kitufe kilichoandikwa ‘like’ ikiwa na maana amesapoti ushindi iliyopata timu hiyo ambayo inahusishwa na mpango wa kumsajili.
Mfumo wa kushambulia unaopendelewa na Kocha Solskjaer umemzindua kila mchezaji kwenye kikosi hicho cha Man United na si Sanchez pekee, ambaye ndio kitu anachokipenda anapokuwa uwanjani, kushambulia tu na si kukaba.
Fowadi huyo wa zamani wa Arsenal, Sanchez alisema: “Wachezaji ni wale wanaotumiwa na Solskjaer ndio waliokuwa wakitumiwa na Jose Mourinho. Lakini kwa sasa tumekuwa bora zaidi kwenye kushambulia na tunakaba pia.
Ukweli ana historia kubwa sana na klabu hii na anapozungumza unahamasika. Falsafa zake ni kugusa mpira mara nyingi zaidi, kutawala mchezo na kufunga mabao.
Sawa unaweza kusema nafasi yake wakati anacheza ilikuwa kwenye ushambuliaji, lakini bado amekuwa akitaka tuwe makini pia tunapokuwa kwenye eneo letu la penalti. Ndio maana tunapata matokeo mazuri. Kitu ambacho kocha alisema ni kuboresha kiwango ni kazi ya mchezaji mwenyewe.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.