Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

WAKATI mwingine mambo huwa hayaendi sawa ndani ya timu. Wachezaji wawili wanajikuta katika uhusiano mgumu na ufikia wakati huwa hawaongei kabisa kwa sababu tofauti za ndani na nje ya uwanja. Wafuatao ni baadhi ya mastaa ambao walicheza timu moja lakini hawakuweza kupiga stori baada ya kutofautiana. Kiburi kinatamalaki.
 
Teddy Sheringham na

Andy Cole

Mastaa wawili wa Manchester United waliotamba vilivyo katika utawala wa Sir Alex ferguson. Wote wawili wana wastani wa kuifungia klabu hiyo kubwa bao moja kila baada ya dakika 84.8. Hata hivyo, Cole na Sheringham walikuwa hawaivi kabisa. Matatizo yao hayakuanzia Old Trafford, hapana, yalianzia katika kambi ya timu ya taifa ya England.
 
ilikuwa ni mechi ya kwanza kwa Cole aliyekuwa kinda na aliingia uwanjani kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Sheringham aliyekuwa ametolewa katika pambano la kirafiki dhidi ya Uruguay. Katika mstari wa kutokea nje ya uwanja, Sheringham aligoma kumpa mkono wa kumtakia kila la kheri Cole na bifu lao likaanzia hapo.
 
Lothar Matthaus na Stefan Effenberg

Wajerumani wawili wababe. Walicheza pamoja katika kikosi cha timu ya Ujerumani na katika klabu yao ya Bayern Munich. Wawili hawa walijulikana kwa kutopendana ndani na nje ya uwanja. Katika pambano la fainali mwaka 1999 kati ya Bayern Munich na Manchester United, Matthaus alikwenda nje ya uwanja na kushindwa kumalizia dakika zote kwa kuwa majeruhi.
 
Hata hivyo, baadaye Effenberg alidai Lothar alikuwa muoga wa mechi tu. katika bifu lao jingine, Effenberg aliwahi kuandika kitabu cha maisha yake ya soka na katika ukurasa mmoja aliandika kichwa cha habari ‘Anachojua Lother Matthaus katika soka’. Cha kushangaza, ukurasa huo aliuacha mtupu bila ya kuandika neno lolote kwa kumaanisha Matthaus hakuna anachojua katika soka.
 
Hata hivyo, baadaye Effenberg alidai Lothar alikuwa muoga wa mechi tu. katika bifu lao jingine, Effenberg aliwahi kuandika kitabu cha maisha yake ya soka na katika ukurasa mmoja aliandika kichwa cha habari ‘Anachojua Lother Matthaus katika soka’. Cha kushangaza, ukurasa huo aliuacha mtupu bila ya kuandika neno lolote kwa kumaanisha Matthaus hakuna anachojua katika soka.
 
Craig Bellamy na John Arne Riise

Mastaa wawili wa zamani wa Liverpool ambao walijikuta katika ugomvi na kutopendana wakati wakiwa katika klabu hiyo. Ilitokea siku moja wakati Liverpool walipokwenda kucheza na Barcelona ugenini, walikwenda katika klabu ya usiku na Riise alikataa maombi ya Bellamy ya kuimba wimbo katika staili ya karaoke. Matokeo yake usiku wake Bellamy alivamia katika chumba ya Riise na kujaribu kupigana naye huku akiwa na fimbo ya mchezo wa gofu.
 
Arjen Robben

na Robert

Lewandowski

Wakati mwingine staili ya soka ya Robben inakufanya umchukie kumtazama. Ni mmoja kati ya wachezaji ambao wana uchoyo mwingi uwanjani. Mara baada ya Robert Lewandowski kuwasili katika klabu ya Bayern haikumchukua muda kukorofishana na Robben kwa jinsi alivyokuwa mchoyo. Uhusiano wao ulidorora ndani na nje ya uwanja.
 
Jens Lehmann na Manuel Almunia

Mara zote Jens Lehmann ambaye alijulikana na mashabiki wa Arsenal kama ‘Mad Jens’ hakupenda kuwa kipa wa pili. Tayari alishakuwa na bifu na kipa namba moja wa timu ya taifa ya Ujerumani wakati huo, Oliver Kahn huku yeye akiwa kipa wa pili. Baadaye akajikuta katika bifu na kipa mwenzake wa Arsenal, Manuel Almunia ambaye alikuwa anasifika kwa kuwa mtu mzuri miongoni mwa wachezaji wa Arsenal.
 
Almunia ambaye ni Mhispaniola aliwahi kukaririwa akidai hakuwa anafahamu kwa nini Lehmann alikuwa na chuki dhidi yake. Hata hivyo, mara kadhaa Lehmann alionekana akimpiga vijembe Almunia hadharani. Siku moja aliwahi kusema “Kukaa benchi dhidi ya mtu ambaye ameanza kucheza soka akiwa na miaka 30 sio kitu cha kufurahisha”. Ilitokea wakati Lehmann alipowekwa benchi na Almunia.
 
Romario and Edmundo

Romario alisajiliwa na Vasco De Gama kwa mara nyingine tena mwaka 1999 huku akitengeneza kombinesheni na staa mwingine wa nchi hiyo, Edmundo ‘The Animal’. Hata hivyo tayari kulikuwa na matatizo kati yao. Hii ilitokana na Romario kuachwa katika kikosi cha Brazil kilichokuwa kinakwenda Kombe la Dunia Ufaransa mwaka 1998 na nafasi yake kuchukuliwa na Edmundo.
 
Romario alikerwa na hali hii na badala yake akabandika picha ya kuchora ya Edmundo akiwa chooni katika mlango wa baa yake Rio De Janeiro. Utani huu ulimkera Edmundo. Wakiwa na Vasco Da Gam walianza kugombana katika vyombo vya habari, pia wakaanza kugombaniwa wanawake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…