Ndiyo maana anaheshimika heshimika sana duniani. Kuna maisha baada ya madaraka [emoji1545][emoji1545][emoji1545]Namkubali sana Generali huyu, mambo aliyoyafanya mwaka 1976 baada ya kuzima mapinduzi yaliyotoa uhai wa Murtala Mohamed, hasa aliporudisha utawala wa kidemokrasia miaka miwli baadaye.
Lakini nimemkubali sana wakati akiongoza Nigeria 1999-2007, kwangu namuona ni mtu aliyefungua ukurasa mwingine wa utawala wa haki ndani ya taifa hilo kubwa lililosheni changamoto mbalimbali barani humu
Sent using Jamii Forums mobile app
Ulikuwa utawala wa kidikteta sana. Mtoto wa Joe Frazier huyu kidogo auliwe na baada ya kichapo hiki aliamua kuachana na ngumi kabisa.
Frank Bruno naye alionja joto ya jiwe...
Hata nguli Larry Holmes naye ilibidi astaafishwe kibabe...
Ulikuwa utawala wa kidikteta sana. Mtoto wa Joe Frazier huyu kidogo auliwe na baada ya kichapo hiki aliamua kuachana na ngumi kabisa.
View attachment 1005774
Nasikia mabondia wengi wakat wa uzee wao huwa wanakuwa na matatizo sana hasa ya ubongo tokana na ngumi hz,,,kuna ukweli hapa bro?Frank Bruno naye alionja joto ya jiwe...
View attachment 1005775
Ni kweli bro. Wengi wao hata kuongea sawasawa hawawezi. Tatizo ni kwamba wengi wao huwa hawastaafu mapema na huendelea kupigana hata baada ya uzee kuwaingia na motor skills kupungua. Mohammed Ali mwenyewe ni mfano mzuri. Ukiangalia pambano lake na Larry Holmes utashangaa jinsi alivyopigwa ngumi nyingi kichwani; na wengi wanaamini kuwa pengine ubongo wake ulivurugwa katika pambano hilo. Akina Sugar Shane Moseley bado wadogo lakini kusikia wanachosema mpaka utege sikio sawasawa. Akina Sugar Ray Leonard na hasimu wake mkuu Tommy Hearns mambo ni yale yale. Ni mchezo mbaya na inabidi uwe na uwezo mkubwa wa kukwepa ngumi na ustaafu mapema kama Mayweather ndiyo ubakie salama. Huyu dogo hajawahi kuwa kwenye pambano ambapo alipigwa ngumi za kichwani na kuumizwa. Mapambano yake karibu yote yeye ni kujilinda kwanza halafu ukizubaa keshakudunda...na amestaafu bila kupigwa...Nasikia mabondia wengi wakat wa uzee wao huwa wanakuwa na matatizo sana hasa ya ubongo tokana na ngumi hz,,,kuna ukweli hapa bro?
Wanataka kupiga hela tena kwa pambano moja la mwishoJuzi kati kwenye game moja ya NBA nafikiri,,Paciano alionekana anasalimiana na The Money Team,,watu wakadai jamaa bado anakumbukumbu juu ya zile ngumi kwenye ule mpambano wao wa kihistoria
Frank Bruno naye kwa sasa yupo yupo tu. Wengi wanaamini hayuko sawa kichwani. Huyu yeye alikuwa hadondoki. Yaani anapigwa tu ngumi mfululizo kama zezeta hajitambui lakini haanguki. Refa asiposimamisha pambano angeweza hata kuuliwa akiwa amesimama tu...Frank Bruno naye alionja joto ya jiwe...
View attachment 1005775
Ni kweli bro. Wengi wao hata kuongea sawasawa hawawezi. Tatizo ni kwamba wengi wao huwa hawastaafu mapema na huendelea kupigana hata baada ya uzee kuwaingia na motor skills kupungua. Mohammed Ali mwenyewe ni mfano mzuri. Ukiangalia pambano lake na Larry Holmes utashangaa jinsi alivyopigwa ngumi nyingi kichwani; na wengi wanaamini kuwa pengine ubongo wake ulivurugwa katika pambano hilo. Akina Sugar Shane Moseley bado wadogo lakini kusikia wanachosema mpaka utege sikio sawasawa. Akina Sugar Ray Leonard na hasimu wake mkuu Tommy Hearns mambo ni yale yale. Ni mchezo mbaya na inabidi uwe na uwezo mkubwa wa kukwepa ngumi na ustaafu mapema kama Mayweather ndiyo ubakie salama. Huyu dogo hajawahi kuwa kwenye pambano ambapo alipigwa ngumi za kichwani na kuumizwa. Mapambano yake karibu yote yeye ni kujilinda kwanza halafu ukizubaa keshakudunda...na amestaafu bila kupigwa...
Mambo ya kugongwa gongwa kichwani ni hatari na wachezaji wa American Footbal, mbali na kuvaa mahelmet nao mambo ni yale yale. Wakistaafu wengi wao wanakuwa hawako sawa kichwani na wanakuja mapema sana. Miaka 60 tu kwisha habari yao...Hata soka nayo sasa wachezaji wanashauriwa kuacha kupiga vichwa mipira hii ya juu kwa sababu madhara yake ni yale yale huko mbele ya safari.