Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kinachoelezwa, Hazard atalipwa mshahara wa Pauni 220,000 kwa wiki ambayo ni sawa na Pauni 11.5 milioni kwa mwaka, lakini kuna bonasi nyingine kiasi cha Pauni 3 milioni, ambazo atalipwa kila msimu kwa muda wa mkataba wake atakaokuwa amesaini kama timu hiyo itabeba La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na Copa del Rey.
 
Wakati hilo la Hazard likiendelea, Los Blancos wana mpango mwingine moto kabisa kwenye meza yao. Mpango huo mpya unazihusu klabu nyingine za Top Six kwenye Ligi Kuu England baada ya Chelsea kuguswa kwenye ishu ya Hazard.
 
Madrid inapanga kufanya biashara na Tottenham Hotspur kuhusu straika Harry Kane kwamba wao wamchukue fowadi huyo na kuwapa Spurs, staa wao wa zamani, Gareth Bale.
 
Los Blancos wao wanataka kuwapa Spurs pesa kiasi cha Euro 120 milioni pamoja na mchezaji Bale ili wao wamchukua Kane, kwenda kumaliza shida yao ya kufunga mabao ambayo kwa sasa imekuwa kubwa tangu Cristiano Ronaldo alipoachana na timu hiyo kutimkia zake Juventus ya Italia.
 
Hilo ndilo lililopo jikoni. Lakini, Madrid pia inacheki chinichini huko Manchester United, ikiwataka mastaa Marcus Rashford na kipa David De Gea, ambao kwa hali ilivyo kwa sasa inaonekana itakuwa ngumu kwa wakali hao kung’oka Old Trafford labda kama tu nguvu ya pesa itatumika.
 
Kuhusu Spurs, Real Madrid hawijamaliza inamtaka pia kiungo Christian Eriksen, ambapo mwishoni mwa msimu kila kitu kitafahamika, huku kukiwa na wasiwasi mkubwa huenda ikavamia pia huko Manchester City kwenda kuchukua huduma ya mastaa wawili, Raheem Sterling na Kevin De Bruyne.
 
Los Blancos wao wanataka kuwapa Spurs pesa kiasi cha Euro 120 milioni pamoja na mchezaji Bale ili wao wamchukua Kane, kwenda kumaliza shida yao ya kufunga mabao ambayo kwa sasa imekuwa kubwa tangu Cristiano Ronaldo alipoachana na timu hiyo kutimkia zake Juventus ya Italia.
 
Liverpool nayo inapambana kuhakikisha inabeba ubingwa msimu huu ili kumzuia staa wake, Mohamed Salah asishawishike wakati Los Blancos itakapopeleka ofa ya kuhitaji saini yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…