Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kicheko ni dawa
Kicheko sehemu muhimu ya maisha yetu ya kila siku.
Kwa mfano ushawahi kumpiga kumbo mwenzako bila kukusudia mkajiapa wote mnacheka?
Wataalamu wanasema mnacheka kwa sababu kila mmoja weno anahisi hakuna aliyemkosea mwenzake.
 
Njia hii ya mawasiliano ilikuwa na ufanisi kwa sababu wahusika walitumia kicheko kuelewana.
Utafiti unaonesha kuwa mara nyingi kicheko hutokana na kauli ya mtu au maoni sio lazima afanye mzaha.
Katika mazungumzo mtu anaecheka mara nyingi huwa anajibu kauli ya mtu bila kutumia maneno.
Kicheko kinaunganisha watu hali ambayo kila muda unavyosonga inadumisha ushirikiano wa kijamii.
 
Utafiti wa hivi karibuni uliyofanywa kuhusiana na kicheko unaashiria kuwa watu wana uwezo wa kutumia vyema njia hii ya mawasiliano wanapotimia umri wa miaka 30 na kuendelea.
Pia unasema kuwa inategemea malezi ya mtu na umri wake; kwa mfano vijana waliyo na usumbufu wa kiakili huenda wasifurahie kucheka wakilinganishwa na vijana wenzao.
Jambo lingine muhimu ni kwamba kicheko husaidia mtu kukabiliana na hali ngumu ya maisha.
 
Utafiti wa hivi karibuni uliyofanywa kuhusiana na kicheko unaashiria kuwa watu wana uwezo wa kutumia vyema njia hii ya mawasiliano wanapotimia umri wa miaka 30 na kuendelea.
Pia unasema kuwa inategemea malezi ya mtu na umri wake; kwa mfano vijana waliyo na usumbufu wa kiakili huenda wasifurahie kucheka wakilinganishwa na vijana wenzao.
Jambo lingine muhimu ni kwamba kicheko husaidia mtu kukabiliana na hali ngumu ya maisha.
 
Watu wanaojadiliana tofauti zao katika mahusiano kwa kutumia kicheko wanaweza kuelewa bila tatizo lolote.
" Jifunze kucheka unapokosea, na jaribu kuona mambo kwa njia nzuri hata wakati hali inapokuwa ngumu."
Hatahivyo hilo litafanikiwa ikiwa wote watafurahia kutaniana hata wakati wamekosana kido kwani hilo ni jambo la kawaida.
Wapenzi wanaotaniana hata wakati wanapopitia hali ngumu whuishi pamoja kwa muda mrefu.
 
Wanafunzi watatu wamekamatwa kuhusiana na mauaji ya mwalimu wao nchini Kenya baada ya kuwapokonya simu.
Peter Omari , mwalimu wa somo la Fizikia katika shule ya upili ya Hopewell mjini Nakuru, alishambuliwa siku ya Alhamisi.
Wanafunzi hawaruhusiwi kuingia shuleni na simu nchini Kenya kwa kuwa hulaumiwa kwa kuzitumia kufanya udanganyifu katika mitihani ya kitaifa mbali na swala la ukosefu wa nidhamu
 
Maafisa wameambia BBC kwamba Omari amekuwa akisimamia masomo ya jioni.
Naibu kaunti kamishna wa eneo hilo Elim Shafi, alisema kuwa bwana Omari alikuwa anarudi nyumbani kwake ndani ya uwa wa shule hiyo yapata kilomita 150 kaskazini magharibi mwa mji mkuu wa Nairobi wakati alipopigwa na kitu katika kichwa.
 
Mashambulio dhidi ya walimu pamoja na shule ni swala lililozua wasiwasi kwa mamlaka kulingana na mwandishi wa BBC Mercy Juma mjini Nairobi.
Mwaka uliopita, mwalimu aliuawa kwa kukatwa na panga na wanafunzi katika eneo la Kisume, Magharibi mwa Kenya baada ya mgogoro katika klabu moja ya burudani.
 
AJALI za barabarani zimeendelea kupukutisha watu, ambapo usiku wa kuamkia juzi Jumamosi Bendi ya Mapacha Watatu inayoongozwa na Jose Mara ilipata pigo kufuatia ajali ya gari kuua mmoja wa wanamuziki wake na kuwaacha wengine wakiwa hoi kwa majeraha.
 
Akizungumza na Mwanaspoti, Jose Mara alisema alipigiwa simu na kuambiwa mwanamuziki wake (Cantona) na wengine wa Max wamepata ajali, ndipo alifunga safari hadi katika tukio kwa ajili ya kutoa msaada.
 
Unajua watu wanachanganya habari, siku hiyo Mapacha haikuwa na shoo, hivyo Cantona alienda kuwapiga tafu Max, hivyo nilipigiwa tu simu kuwa kuna ajali imetokea ndio tukatoka tukaenda kuwachukua kuwapeleka Lugalo, lakini pale walihamishiwa Muhimbili, mwanamuziki wangu alifia njiani,” alisema Mara.
 
Katika ajali hiyo, kila mtu anasema lake kuhusu watu waliokuwa kwenye gari ambalo limepata ajali, ila hadi sasa majeruhi wametambulika ni wanne na waliofariki ni wawili ambao ni Cantona na Zai na watu wakaribu waliowahi kuona ajali hiyo wamedai gari lililokuwa na wanamuziki liligongwa na gari lingine ambalo lilihama njia na kwenda upande wao,” alisema Jose Mara
 
Mara aliwataja wengine wliojeruhiwa ni Max, Sweet Baby na , Yaniki Solo na mpiga solo na Sele Kadanse.

Marehemu Cantona a.k.a ‘Mugogo wa Mazizini ‘aliwahi kupitia bendi ya Diamond Musica Intertnational na kuweza kutamba na Wimbo wa ‘Acha Kulia’ katika alibamu ya Tindi Kali ya Mwaka.
 
Mapema mchana wanamuziki na wadau wa fani hiyo waliitana Ukumbi wa Vijana kwa nia ya kuunda Kamati ya Mazishi ya wenzao walitangulia mbele ya haki na kusababisha msiba mkubwa katika muziki wa dansi. Mwanaspoti lilimsaka kwa simu Kamanda wa Mkoa wa Kinondoni, Jumanne Mlilo lakini hakuweza kupatikana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…