4.Gianluigi Buffon- PSG
Paris Saint-Germain kipa wao namba mbili, Gianluigi Buffon anafurahia maisha kwenye kikosi cha wababe hao wa Ufaransa pengine kuliko makipa wengine wote namba mbili huko Ulaya. Hilo linatokana na kwamba karibu amecheza mechi idadi sawa na kipa chaguo la kwanza kwenye kikosi hicho cha PSG, Alphonse Areola. Kipa huyo gwiji wa Italia, Buffon amejiunga na wababe hao wa Ligue 1 kwenye dirisha lililopita la majira ya kiangazi katika kipindi ambacho wengi waliamini kwamba angetangaza kustaafu soka baada ya kupata mafanikio makubwa katika kikosi cha Juventus. Lakini, ameamua kuendelea kucheza na sasa anampa wakati mgumu kipa Areola huko kwenye kikosi cha PSG kwa sababu ya kwamba yeye ni namba mbili, lakini anapata nafasi ya kucheza kushindana na namba moja. Kumekuwa na ripoti kwamba PSG ipo tayari kumpa ofa ya mkataba mwingine wa mwaka mmoja.