Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kwamba, unahitaji kuwa na washambuliaji makini kufunga mabao ili timu kushinda mechi yake, lakini utahitaji mabeki makini kulinda ushindi huo uliopatikana na matokeo ya jambo hilo likifanikiwa, basi timu husika utakuwa imeshinda ubingwa unaoshindaniwa.
 
Hapo kwenye kulinda ushindi uliopatikana, kuna mtu mmoja ni muhimu sana na huyo ni golikipa. Kwenye soka unaambiwa kwamba unahitaji kuwa na kipa mahiri kurahisisha kazi ya kubeba mataji. Ukibisha hilo, nenda kawaulize Liverpool kwa kile alichowafanyia kipa wao kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid Mei mwaka jana. Makipa ni muhimu kwelikweli na ndio maana baada ya hapo, Liverpool ikavunja benki kwenda kunasa huduma ya kipa wa Kibrazili, Alisson Becker. Msimu huu maisha ni safi kabisa huko Anfield.
 
5.Petr Cech- Arsenal

Kipa wa Arsenal, Petr Cech ametangaza kwamba itakapofika mwisho wa msimu huu atang’atuka kwenye soka na kustaafu. Kipa huyo wa zamani wa Chelsea ameshinda karibu matajiti kwenye ngazi ya klabu katika maisha yake ya soka. Anashikilia pia rekodi ya kucheza mechi nyingi bila ya kuruhusu wavu wake kuguswa kwenye Ligi Kuu England.
 
Cech usalama wa nafasi yake kwenye kikosi cha Arsenal umeingia kwenye mashaka makubwa baada ya kocha Unai Emery kumsajili kipa Bernd Leno na kumfanya kuwa namba moja wake. Gwiji huyo wa Jamhuri ya Czech, Cech aliona kwamba hana nafasi tena ya kushindania namba hasa baada ya kutambua kwamba umri wake ni miaka 36. Hata hivyo, hata akiamua kutengua uamuzi wake wa kustaafu na kuendelea kucheza soka, kuna klabu nyingi tu zitahitaji huduma yake kwa sababu bado ana uwezo mkubwa wa kuanza kwenye mechi kuliko namba moja wake, Leno.
 
4.Gianluigi Buffon- PSG

Paris Saint-Germain kipa wao namba mbili, Gianluigi Buffon anafurahia maisha kwenye kikosi cha wababe hao wa Ufaransa pengine kuliko makipa wengine wote namba mbili huko Ulaya. Hilo linatokana na kwamba karibu amecheza mechi idadi sawa na kipa chaguo la kwanza kwenye kikosi hicho cha PSG, Alphonse Areola. Kipa huyo gwiji wa Italia, Buffon amejiunga na wababe hao wa Ligue 1 kwenye dirisha lililopita la majira ya kiangazi katika kipindi ambacho wengi waliamini kwamba angetangaza kustaafu soka baada ya kupata mafanikio makubwa katika kikosi cha Juventus. Lakini, ameamua kuendelea kucheza na sasa anampa wakati mgumu kipa Areola huko kwenye kikosi cha PSG kwa sababu ya kwamba yeye ni namba mbili, lakini anapata nafasi ya kucheza kushindana na namba moja. Kumekuwa na ripoti kwamba PSG ipo tayari kumpa ofa ya mkataba mwingine wa mwaka mmoja.
 
3.Jasper Cillessen- Barcelona

Barcelona ina makipa wawili wa kiwango cha juu kabisa. Na kwamba inachokifanya ni kuwafanya makipa wote hao wawili kuwa na furaha. Kipa namba moja, Marc-Andre ter Stegen atadaka kwenye mechi zote za La Liga na Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati Jasper Cillessen anakuwa golini kwenye mechi za Copa del Rey. Hata hivyo, wachambuzi wa mambo ya soka wamekuwa wakimshangaa kipa huyo ambaye ni namba moja huko kwenye timu ya taifa ya Uholanzi anakubali kuendelea kubaki Nou Camp, wakati anacheza mechi chache sana. Ukweli ni kwamba Cillessen ni rahisi sana kwake kupata timu ya kwenda kuanza katika kikosi cha kwanza kama ataamua kuihama Barcelona.
 
2.Sergio Romero- Man United

Kipa namba moja wa Argentina, Sergio Romero hakuna ubishi ni mmoja wa makipa bora kabisa duniani kwa sasa. Louis Van Gaal alimsajili kwa uhamisho wa bure kabisa mwaka 2015 baada ya mkataba wake kufikia kikomo huko Sampdoria. Lakini, kipa Romero ameshindwa kumpoka namba David De Gea kwenye goli la Manchester United. Ijumaa iliyopita alikaa golini wakati Man United ilipocheza na Arsenal na hakika kiwango chake kilikuwa moto. Aliokoa hatari kadhaa katika kipindi cha pili kuwagomea Arsenal kusawazisha kabla ya timu yake kumaliza mechi hiyo kwa kufunga bao la tatu. Alikuwa golini wakati Man United ilipoichapa Ajax kwenye fainali ya Europa League mwaka 2017.
 
1.Keylor Navas- Real Madrid

Tangu kipa Keylor Navas alipowasili Real Madrid msimu wa 2014/15, timu hiyo imebeba mataji 11 ikiwamo matatu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Katika kipindi hicho, kipa huyo raia wa Costa Rica, amecheza mechi 152. Klabu ilitaka kumsajili David De Gea, lakini dili hilo lilikwama mwaka 2015.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…