Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

LIGI Kuu England huko moto unawaka. Liverpool usiku wa jana Jumatano walikuwa na fursa ya kuongeza pengo la pointi kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo baada ya timu inayowafukuzia Manchester City kukutana na kipigo kutoka kwa Newcastle United cha mabao 2-1.
 
5.Yerry Mina vs Burnley, sekunde 99

Beki wa kati, Yerry Mina jina lake ameliweka pazuri kwenye Ligi Kuu England kutokana na kuwa miongoni mwa wafungaji wa mabao ya mapema sana kwenye ligi hiyo msimu huu. Yerry Mina alifunga sekunde ya 99 wakati Everton ilipomenyana na Burnley. Bao hilo la Yerry Mina lilikuwa la 7,000 kufungwa na Everton kwenye mchakamchama wa Ligi Kuu England. Hiyo ilikuwa Desemba 26 mwaka jana wakati beki huyo anayecheza Goodison Park kwa mkopo akitokea Barcelona, aliweka alama zake kwenye ligi hiyo kwa kufunga bao la mapema dhidi ya Burnley. Bao hilo lilifungua ukurasa mzuri wa mabao kwa kikosi hicho cha kocha Marco Silva kwani hadi mwisho wa mchezo, kikosi cha Everton kilipiga mtu Bao 5-1.
 
4.Leroy Sane vs Fulham, sekunde 90

Septemba 15 mwaka jana, winga wa Kijerumani, Leroy Sane aliifungia bao Manchester City kwenye sekunde ya 90 tu katika mechi dhidi ya Fulham iliyofanyika uwanjani Etihad. Bao hilo lilianzisha mwanzo mzuri kwa mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu England kwa sababu walimaliza mechi hiyo wakiwa wameshinda mabao 3-0.

Sane alifunga bao lake la kwanza baada ya kusubiri kwa muda mrefu ikiwa mwanzoni mwa msimu alianza kwa kuwekwa kando kwenye baadhi ya mechi huku ikielezwa alikuwa kwenye shida na kocha wake huko Man City, Pep Guardiola.
 
3.Andre Gray vs Fulham, sekunde 87

Bao alilofunga Andre Gray kwenye mechi dhidi ya Fulham la sekunde ya 87 kwenye Ligi Kuu England ni la pili kufungwa na Watford kwenye ligi hiyo baada ya lile alilofunga, Etienne Capoue dhidi ya Leicester City Novemba 2016, alipofunga kwenye sekunde ya 32. Kwa msimu huu, Gray alifunga bao lake Septemba 22 mwaka jana.
 
Andre Gray aliwashtusha Fulham kwa bao hilo la mapema kuwafanya Watford kuwa mbele kwa bao lao hilo. Hata hivyo, Watford ilishindwa kutambana kulilinda bao lao la mapema kabisa la sekunde 87, kwani Fulham walisawazisha na kufanya mchezo huo kumalizika kwa sare.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…